0 0
Read Time:37 Second
Baadhi ya Watanzania pichani wakisubiri kumsalia marehemu

Kwa uwezo wa Allah na ushirikiano wa hali ya juu uliopo kati yetu (watanzania wa ugiriki) tumeweza kufanikisha mchango wa kumsafirisha mwenzetu SAIDI HASSAN MGOI (Maarufu kwa jina la CHANCE) ili akazikwe nyumbani. Mwili wa Marehemu utawasili Dar J’mosi13/08 saa NANE NA NUSU USIKU kwa ndege ya shirika la Uturuki.

Marehemu alikoshwa,alikafiniwa na kuswaliwa katika msikiti wa ELSALAAM uliopo Neos Kosmos Athens.Idadi kubwa ya watanzania walihudhuria msikitini.
Taarifa tulizo nazo khs maziko yatafanyika J’pili 14/8 saa saba mchana Tandika Mikoroshini kwa SANDARI ila kwa maelezo kirefu fanyeni mawasiliano na FATUMA dada yake (0718567537) au (0783694736)

Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin.

INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN

Kayu Ligopora

KATIBU wa JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI

WABONGO UGHAIBUNI
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %