
Hassan Ng’anzo afariki kwa ajali ya gari akiwa Tanzania
Mitandao ya wana diaspora duniani imegubikwa na huzuni mkubwa baada ya kuondokewa na kiungo muhimu veterani wa Diaspora. Hassan Ng’anzo ni Diaspora aliyekuwa akiishi nchini Norway.
Taarifa za msiba zilitufikia kwa njia ya mawasiliano kutoka kwa wadau mbalimbali ambao walitaka kujua ukweli wa taarifa. Wabongo ughaibuni media iliwasiliana moja kwa moja na kaka wa marehemu ambae alithibitisha taarifa za msiba.
Marehemu ameacha Mke na Watoto wawili nchini Norway, ambao wanategemewa kuwasili kesho siku ya Alhamisi jijini Daressalaam kwa ajili ya kushiriki mazishi. Marehemu atazikwa siku ya ijumaa kama ilivyo elezwa kwenye taarifa na ratiba kutoka kwa familia.








