0 0
Read Time:1 Minute, 36 Second

Bologna Italy

Na Kagutta Maulidi | Italy

Kampuni ya uchapishaji ya kitanzania APE NETWORK imeshiriki maonyesho makubwa ya kimataifa ya vitabu vya watoto nchini Italy. Maonyesho hayo ya 63 ya vitabu vya watoto Bologna Children’s Book Fair (BCBF), yalifanyika kuanzia tarehe 13 -16 mwezi huu wa aprili 2026 jijnini Bologna.

Kampuni pekee ya uchapishaji ya Ape Network aliwakilishwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo ndugu Hermes Damian Salla .

Tukio hilo la maonyesho linaloongoza duniani kwa uchapishaji wa vitabu vya watoto, liliitambua Norway kama mgeni rasmi wa maonyesho ya BCBF 2026 . Maonyesho hayo yamefanyika pamoja tamasha la “BOOM! Crescere nei libri”, ambalo linaangazia zaidi ya matukio 150.

Ushiriki huu umewezekana kutokana na usaidizi wa ITA – Shirika la Biashara la Italia na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Italia – MAECI, inayolenga kukuza fursa za biashara kati ya wachapishaji wa kitaifa na kimataifa. Mojawapo ya mipango muhimu zaidi ni programu kubwa ya mwaliko inayounga mkono ushiriki katika maonyesho ya wataalamu zaidi ya 150 kutoka kote ulimwenguni. BCBF ni maonyesho yenye kutoa fursa kubwa kwa wadau wa sekta ya uchapishaji ,mawakala na waandishi kukutana.

Napoli Italy

Pia mkurugenzi wa APE NETWORK alipata fursa ya mualiko katika chuo kikuu cha Orientale cha jijini Napoli ambapo alishiki katika mada inayohusu Uchapishaji kama Njia ya Kuhifadhi na Kudumisha Ustaarabu na Sanaa za Kiafrika.

Tukio hilo la Fasihi katika Lugha za Kiafrika na Uchapishaji( Letteratura in lingue Africane e editoria) lilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo kikuu cha Orientale Napoli lilisimamiwa na kuongozwa na Profesa Gaudioso Roberto PhD na Profesa Aiello Flavia PhD kutoka chuo kikuu cha Orientale Napoli.

Tukio la fasihi katika lugha za kiafrika na uchapishaji lilifunguliwa na Dkt. Gala Maria Follaco Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Asia, Afrika, na Mediterania (DAAM) Chuo Kikuu cha Naples “L’Orientale”.

Mkurugenzi wa Ape Network Hermas Damian Salla akiwa na Profesa Gaudioso Roberto PhD, wakati akitoa mada chuo kikuu cha Orientale Napoli

Matukio maonyesho ya vitabu Bologna Italy

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %