0 0
Read Time:1 Minute, 25 Second

โ–ช๏ธ๐™€๐™ ๐™ ๐™ช๐™ฌ๐™š๐™ ๐™š๐™ฏ๐™– ๐™€๐™ช๐™ง๐™ค ๐™ข๐™ž๐™ก๐™ž๐™ค๐™ฃ๐™ž 50 ๐™ ๐™ช๐™จ๐™–๐™ž๐™™๐™ž๐™– ๐™ ๐™ช๐™ฉ๐™ค๐™ ๐™ค๐™ข๐™š๐™ฏ๐™– ๐™จ๐™ค๐™ฉ๐™ค๐™ ๐™– ๐™—๐™–๐™ง๐™–๐™ฃ๐™ž ๐˜ผ๐™›๐™ง๐™ž๐™ ๐™–

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na FAO, Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH), Umoja wa Afrika, jumuiya za kikanda na wadau wengine katika kuimarisha uwekezaji na mifumo ya kudhibiti magonjwa ya mifugo kwa lengo la kuchangia kutokomeza Sotoka ifikapo mwaka 2040.

โ€œTunataka kuona uwekezaji wenye nguvu zaidi, unaotabirika na endelevu. Umiliki wa kitaifa na ufadhili wa ndani lazima viwe msingi, vikisaidiwa na FAO, WOAH, Umoja wa Afrika, jumuiya za kikanda, taasisi za fedha za kimataifa, washirika wa maendeleo na sekta binafsi.โ€

โ€œTunapaswa kuondoka katika hatua zilizotawanyika na kuelekea kwenye mifumo ya kudumu; kutoka mipango ya kitaifa pekee kwenda ushirikiano wa kikanda; na kutoka ahadi kwenda kwenye matokeo yanayoweza kupimika,โ€ alisisitiza Waziri Mkuu.

Alisema hayo jana, (Jumanne, Septemba 22, 2026) jijini Roma, Italia, wakati akishiriki mjadala wa ngazi ya juu kuhusu uwekezaji katika kutokomeza Sotoka na kudhibiti Ugonjwa wa Miguu na Midomo kwenye Mkutano wa Kimataifa ulioandaliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kuhusu utekelezaji wa Afya Moja katika mifumo ya chakula na kilimo.

Alisema chanjo pekee haitoshi, bali Tanzania inahitaji maabara zinazofanya kazi, mifumo madhubuti ya ufuatiliaji, usambazaji wa chanjo wa uhakika, utambuzi wa mifugo, wataalamu wenye ujuzi na ushirikiano baina ya nchi na nchi hasa kwenye maeneo ya mipakani.

Akizungumzia umuhimu wa ushirikiano wa kikanda, Dkt. Mwigulu alisema magonjwa ya mifugo hayaheshimu mipaka ya nchi, na kubainisha kuwa wakati nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikijadili hatua za kuelekea shirikisho, wanyama tayari wameungana kwa kasi zaidi.

โ€œWakati nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikiendelea kujadili namba ya kuingia katika mfumo wa shirikisho, wanyama tayari wameungana haraka kuliko sisi,โ€ alisema.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %