
Ubalozi wa Tanzania nchini China umeandaa Mkutano Maalum kwa madhumuni ya kuyakutanisha Makampuni ya Tanzania yanayouza Mabondo ya Samaki (dry fish belly products) na Kampuni ya Alibaba Group ya China. Mkutano huo utafanyika kwa njia ya mtandao wa ZOOM Jumanne tarehe 22 Desemba 2020 kuanzia saa 3 asubuhi..Makampuni ya Tanzania yenye nia ya kushiriki yanaombwa kuwasiliana na Ubalozi kwa barua pepe: beijing@nje.go.tz; whatsup +86 186 1424 7590 kati ya leo na jumatatu ili kujiandikisha kushiriki katika mkutano huo…Share na wenzako