
Tanzania imejivunia mafanikio iliyoyapata katika kipindi cha miaka 40 ya uanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ameyataja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na miaka 40 ya uanachama wa SADC tangu 1979, lugha ya kiswahili kutumika katika mikutano yote ya kisekta ya SADC pamoja na kutengenzwa sanamu maalumu ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
“Pamoja na mambo mengine, mkutano wetu wa leo wa Baraza la Mawaziri wa SADC tunategemea kujadili masuala mbalimbali anayohusu jumuiya hiyo likiwemo suala la matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mikutano yote ya kisekta,” Amesema Prof. Kabudi.
Mambo mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na suala la kutengeneza sanamu maalumu ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambapo sanamu hiyo itawekwa katika jengo la Amani Addis Ababa nchini Ethiopia, pamoja na maadhimisho ya miaka 40 ya SADC.
“Hivyo kupitia mkutano huu tutakamilisha mchakato wa kumpata mtu atakae ifua sanamu hiyo ya Mwl. Nyerere ambapo itawekwa katika jingo la Amani Ethiopia,” Amesema Prof. Kabudi
Prof. Kabudi ameendelea kueleza kuwa katika mkutano huo suala la maadhimisho ya miaka 40 ya SADC pia limejadiliwa ikiashiria umoja wa SADC kudumu kwa miaka 40. READ MORE