Ilikuwa siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita tarehe 20/03/2021 Watanzania nchini Italy walikutana Ubalozini kwa ajili ya sala na maombi kufutia kifo cha aliekuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli. Ghafla hiyo ya maombolezo na sala ilihitimishwa kwa hotuba fupi ya kuwashukuru Watanzania waliowakilishi wengi ambao kwa sababu za hali ya maradhi ya corono haikuwezekana kujumuika wengi kwa pamoja.Mh Balozi George Madafa aliwashukuru wote kwa moyo wao na mapenzi waliyoonyesha kwa kutoka mbali na kuja kujumuika wote katika tukio la msiba mkubwa.
Read Time:31 Second