
Na:
Babu Stanley Otto Mayunga [Ndebire]
0621014417
Tayari hatua zimechukuliwa dhidi ya gazeti la UHURU baada ya kuchapisha taarifa iliyonukuu maneno ambayo hayakutamkwa na Rais wa JMT Ndg. Samia S. Hassan.Jambo hili lingefanywa na chombo kingine cha habari ingekuwa ni habari tu na pengine kuitwa propaganda lakini kuandikwa na gazeti linalomilikiwa na chama tawala [CCM] kunafanya iwe habari ya kusisimua na hatuna budi kujifikirisha zaidi.
Najaribu kubeba uhusika wa Mkurugenzi,mhariri na msimamizi na kuwa upande wa kilichotokea ni kutafsirika vibaya.Lakini njia pekee ya kuthibitisha hili ni kujiuliza:
Je,lugha iliyotumika “sษชษดแด แดกแดแดขแด แดแดแดกแดษดษชแด แดสแดษชs 2025” ni ngumu kiasi cha wasomaji kushindwa kuitafsiri au sentensi hiyo ina maana ipi nyingine?Kwa nini isingekuwa “sษชแดแดแดกแด ษดแด แดกแดแดขแด สแด แดแดแดกแด สแดษชs 2021” kama alivyosema mwenyewe?Je kuna mtu au hatua miongoni mwa mlolongo mrefu wa uhakiki wa habari kabla haijachapishwa ilirukwa [alirukwa] yaani itifaki ya uhariri haikufuatwa?Je,mama Samia aliyasema maneno hayo?Kwa nini habari ikaandikwa na gazeti moja tu ukizingatia uzito wa hoja yenyewe na hasa kutoka kwa Rais?
Majibu ya maswali haya na mengine yananipa ukakasi kushindwa kuhalalisha ubahati mbaya katika jambo hili.
Katika mahojiano ya Rais na BBC kwa lugha zote za kiswahili na kiingereza,Rais hajatamka chochote kuhusu mpango wa urais 2025.Kilichofanyika ni upotoshaji wa maudhui ya maelezo yake.
Rais angetamka maneno hayo hakika ingekuwa habari motomoto katika vyombo vingi vya habari na hata ndani ya CCM kwenyewe.Lakini nini hasa lilikuwa lengo la wahusika katika upotoshaji huu!
Je,ni kutuliza hali ya kisiasa hasa ndani ya CCM na kumpa mama fursa kufanya kazi zake kwa utulivu?Je,ni kumuandaa Rais kisaikolojia ili aridhike na kipindi kimoja na kutoa fursa ya kuchipuka kwa makundi na kuandaa safu zao?Je,ni kuleta mgogoro ndani ya chama na kukwamisha shughuli za Rais na kwa maslahi ya nani au kundi lipi linalo ratibu upuuzi huu?Je,ilikuwa mbinu ya kibiashara kuvutia wanunuzi ilhali madhara yake yakipuuzwa?Je,ni dharau na kumpima imani Rais na M/kiti wa chama au ni uzembe hasa wa kutosikiliza vizuri mahojiano?
Mama Samia amekuwa Rais wetu kwa mujibu wa ibara ya 37[5] ya katiba ya JMT.Na katiba hiyo ibara ya 40[4] inaeleza kuwa:
๐๐ป๐ฑ๐ฎ๐ฝ๐ผ ๐ ๐ฎ๐ธ๐ฎ๐บ๐ ๐๐ฎ ๐ฅ๐ฎ๐ถ๐ ๐ฎ๐ป๐ฎ๐๐ต๐ถ๐ธ๐ฎ ๐ธ๐ถ๐๐ถ ๐ฐ๐ต๐ฎ ๐ฅ๐ฎ๐ถ๐ ๐ธ๐๐ฎ ๐บ๐๐ท๐ถ๐ฏ๐ ๐๐ฎ ๐บ๐ฎ๐๐ต๐ฎ๐ฟ๐๐ถ ๐๐ฎ ๐ถ๐ฏ๐ฎ๐ฟ๐ฎ ๐๐ฎ 37[5] ๐ธ๐๐ฎ ๐ธ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ป๐ฑ๐ถ ๐ธ๐ถ๐ป๐ฎ๐ฐ๐ต๐ผ๐ฝ๐๐ป๐ด๐๐ฎ ๐บ๐ถ๐ฎ๐ธ๐ฎ ๐บ๐ถ๐๐ฎ๐๐ ๐ฎ๐๐ฎ๐ฟ๐๐ต๐๐๐ถ๐๐ฎ ๐ธ๐๐ด๐ผ๐บ๐ฏ๐ฒ๐ฎ ๐ป๐ฎ๐ณ๐ฎ๐๐ถ ๐๐ฎ ๐ฅ๐ฎ๐ถ๐ ๐บ๐ฎ๐ฟ๐ฎ ๐บ๐ฏ๐ถ๐น๐ถ,๐น๐ฎ๐ธ๐ถ๐ป๐ถ ๐ธ๐ฎ๐บ๐ฎ ๐ฎ๐ธ๐ถ๐๐ต๐ถ๐ธ๐ฎ ๐ธ๐ถ๐๐ถ ๐ฐ๐ต๐ฎ ๐ฅ๐ฎ๐ถ๐ ๐ธ๐๐ฎ ๐บ๐๐ฑ๐ฎ ๐๐ฎ ๐บ๐ถ๐ฎ๐ธ๐ฎ ๐บ๐ถ๐๐ฎ๐๐ ๐ฎ๐ ๐๐ฎ๐ถ๐ฑ๐ถ ๐ฎ๐๐ฎ๐ฟ๐๐ต๐๐๐ถ๐๐ฎ ๐ธ๐๐ด๐ผ๐บ๐ฏ๐ฒ๐ฎ ๐ป๐ฎ๐ณ๐ฎ๐๐ถ ๐๐ฎ ๐ฅ๐ฎ๐ถ๐ ๐บ๐ฎ๐ฟ๐ฎ ๐บ๐ผ๐ท๐ฎ ๐๐.
Hivyo mama Samia anaruhusiwa kugombea tena mara moja [2025-2030] kwani ameshika Urais ikiwa imebaki zaidi ya miaka mitatu.Na kwa utaratibu wetu wa CCM wala hatuna nongwa katika hilo kwani mwenyekiti wetu au Rais anayetokana na CCM lazima amalize vipindi vyake viwili.
Mama katuvusha katika kipindi kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa kiongozi wetu.Katika baadhi ya nchi,kipindi kama hicho wameshuhudia machafuko yanayotokana na makundi ya wafuasi kwa kuamini kiongozi aliyefariki alikuwa bora kuliko aliyepo na kinyume chake au walau kwa mgogoro wa kikatiba.
Si tu gazeti bali gazeti la UHURU linalomilikiwa na CCM linatakiwa liwe kiongozi na kuonyesha weledi na utii wa sheria,kanuni,maadili na uadilifu.Ikumbukwe chokochoko za kidini na propaganda za vyombo vya habari vimezivuruga nchi nyingi na kuondoa amani na utulivu kwa mfano Rwanda wakati wa mauaji ya kimbali.Ni hatari sana gazeti la CCM kutumika kuudanganya umma juu ya kiongozi wa CCM.
Hivyo kama kuna mkakati wa njama za hujuma dhidi ya Rais wetu na serikali yake basi hatua zisiishie kuwafuta kazi hao watatu bali upekuzi zaidi ufanyike kuugundua mtandao wote kama upo na hatua kali zichukuliwe.
Hayati Magufuli aliwahi kusema hatoongeza hata sekunde baada ya muda wake wa urais kuisha.Nashauri,nguvu iliyotaka kutumika kumtaka aongeze muda kinyume na katiba ni vema tukaielekeza katika kuungana na Rais Samia kuhakikisha anamaliza vipindi vyake viwili kwa mujibu wa katiba.
Kama wapo na bila shaka wapo waliojipanga kumrithi hayati Magufuli basi lazima wawe wapole,wakubaliane na matokeo na wavute subira kwani kila jambo jema linakuja ndani ya muda muafaka.Chondechonde tusipeane mzigo wa kuanza kukitetea chama kwa matatizo ya kujitakia.
Wana CCM tujikite kuihoji serikali,kukosoa na kuboresha mambo muhimu ya utekelezaji wa ilani yetu.Tumuache Rais afanye kazi ya kuwatumikia watanzanzia kwa moyo mmoja.Tusisahau tulivyokuwa wahanga wa makundi na mitandao almanusra chama kitufie.
Ni kweli alisema hakutarajia kuwa Rais kwani siku zote alimuomba M.Mungu wamalize salama ngwe yao yeye na hayati Magufuli na kuwapisha wengine.Lakini binaadamu tunapanga na M.Mungu anaamua.Sasa keshakuwa,tulihitaji atuache kama yatima au tulihitaji machafuko na nchi isikalike au hata mapinduzi kutoka kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama?
Tumuache mama akiona agombee tena si dhambi kwani katiba inamruhusu kama nilivyoandika hapo awali.Na akiamua pia kuwaachia urais na urafi wenu wa madaraka ni maamuzi na haki yake pia.
lakini tukumbushane tu hakuna mwenye hati miliki ya uongozi wa nchi.Nchi hii ni yetu sote na Mungu umuinua amtakaye miongoni mwetu.Hivyo uhuni wowote wa kutaka kutuvuruga tusiukaribishe wala kuuendekeza.Tumewahi kusema aongoze mpaka achoke leo tunashindwaje kusema aongoze mpaka amalize muda wake kama si hiana!
Naomba nimtangulize Mungu ninapomnukuu Rais wetu:
๐๐๐ญ๐๐ง๐ณ๐๐ง๐ข๐ ๐ฐ๐๐ฆ๐๐ง๐ข๐๐ฅ๐๐ฐ๐ ๐ค๐ฎ๐ก๐ฎ๐ฌ๐ฎ ๐ญ๐จ๐ณ๐จ ๐ง๐ ๐ฌ๐ก๐ข๐๐ ๐ฒ๐๐จ ๐ง๐ข ๐ค๐ข๐ฐ๐๐ง๐ ๐จ ๐ค๐ฎ๐ฐ๐ ๐ค๐ข๐ค๐ฎ๐๐ฐ๐.
Kweli tumekuelewa mama unahitaji fedha kwa ajili ya barabara,maji,umeme,afya,elimu n.k. lakini japo umechelewa basi sasa fanya maamuzi kuliko kutofanya kabisa juu ya jambo hili.Tunaumia na hatuhitaji kwenda Burundi.
Leo ni siku ya vijana duniani [Agosti 12,2021].Tunasubiri kusikia kauli na mikakati ya matumaini.








