0 0
Read Time:3 Minute, 41 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
August 21,2021.

Waziri wa fedha wa Tanzania Mh Mwigulu Nchemba jana sio kwamba ameibua mjadala mpya na mkubwa mitandaoni na kwenye taarifa za habari za vituo mbalimbali vya televisheni nchini baada ya kuja na hoja ya makusanyo yaliyopatikana tangia kuanza kwa utekelezaji wa sheria hiyo hivi karibuni!

Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Mwigulu Nchemba ndio injini ya kuanda na kutekeleza mipango ya kitaifa ya kimaendeleo Nchini lakini Waziri na timu yake pale wizarani wanapaswa kujua jinsi ya “kubalance”mambo makuu mawili;

1.Wizara na Waziri husika wanabeba mipango ya Serikali ya kuondoa umasikini wa kipato kwa Watanzania kwa kuiwezesha mipango mbalimbali ya kuondoa umasikini”capital formations”kupitia programu mbalimbali!

Ndio maana chini ya Wizara hii mipango na programu mbalimbali za kukuza uchumi na kuondoa umasikini zinaratibiwa na miongoni mwa programu hizo ni programu kama za tasaf,Banki ya kilimo,mifuko mbalimbali ya uwezeshaji wananchi katika ngazi kuanzia ya kitaifa mpaka ngazi za Mikoa Wilaya!

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imekuwa ikitoa na ikipelekea fedha mbalimbali kwa wananchi kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa mitaji”capital formation” ili watu waweze kufanya miradi ya kuzalisha mali kwa makundi mbalimbali!

2.Wajibu wa Wizara ya Fedha na Mipango pia uhusika na kupendekeza vyanzo vipya vya mapato na kuvitekeleza kwa lengo la kukusanya mapato ya Serikali kupitia taasisi za TRA na taasisi zinginezo!
Hapa Serikali yetu inapaswa kuwa makini sana katika kukusanya kodi na tozo zinazotokana kwa wananchi bila kuzohofisha juhudi zake yenyewe na kuondoa umasikini!

JE,SERIKALI INAKOSA JICHO LA TATU KWENYE MASUALA YA KUPUNGUZA UMASIKINI NCHINI?

1.Lengo kuu la Serikali la kuanzisha programu mbalimbali za kuondoa umasikini nchini lilikuwa kutimiza lengo la kuweza kujibu mipango mikubwa ya kitaifa ya mkukuta,mkurabita na mkuza ili kupunguza umasiki kwa watu wake!Takwimu za hivi karibuni kutoka NBS zinaonyesha kupungua kwa umasikini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja kutokana na utekelezaji wa programu za mbalimbali zikiwemo programu za tasaf,Banki ya kilimo na mikopo mbalimbali!

Lengo hapa la Serikali ilikuwa ni kutengeza mitaji”capital formation” kwa wananchi masikini kupitia mikopo,ruzuku kwa lengo la kupunguza umasikini wa kipato kwa Watanzania!

2.Kitendo cha serikali kuamua kuanzisha utitiri wa tozo na kodi mbalimbali katika mwaka huu wa fedha sio tu kunachochea kuongezeka kwa umasikini wa kipato hivyo kubeza shughuli za Serikali yenyewe!

Hii ni hatari kwa juhudi za Serikali za kuondoa umasikini wa kipato Nchini!Tozo za miamala ya simu,tozo za majengo,tozo za mafuta,na tozo nyingine nyingi sio tu kwamba zinaua mitaji bali pia zinaua uwezo wa watu kurudisha mikopo hasa ya kibenki kwa sababu tozo hizi zinaongeza gharama za kuendesha biashara na shughuli za ujasiliamali Nchini!.

3.Mkanganyiko huu sio tu kwamba unaweza “kupararise” Uchumi na shughuli za uzalishaji ambazo zilianza kukua Nchini bali pia kunaweza kuuwa uwezo wa wajasilimali wadogo kurudisha mikopo katika mabenki kutokana na kupanda kwa gharama za kuendesha shughuli za ujasiliamali na uzalishaji!mfano,Kijana mwenye mtaji wa Tshilingi 100,000 endapo atapitisha fedha yake kupitia miamala anakatwa mpaka kufikia Tsh 6000+ ambayo ndio labda faida yake baada ya kufanya mauzo ya biashara yake kwa siku!

Mwisho,lazima tuamue je,tunahitaji kuona Serikali yenye ukwasi au tuwe na wananchi wenye ukwasi?Maendeleo ya Nchi yoyote uanzia kwa watu kuwa na uwezo wa kutengeneza fursa mpya za uzalishaji kupitia mitaji yao”capital formation”.

Taifa ambalo watu wake hawana uwezo wa kutengeneza mitaji na kuikuza mitaji hiyo, kamwe halitoweza kupiga hatua yoyote!Napenda kumnukuu mchumi nguli duniani alipoelezea suala la kwanini jamii nyingi ni duniani ni masikini.

Nurke’s Vicious Cycle of Poverty Theory inasema kuwa, tatizo kubwa la jamii nyingi duniani ni kukosa kuwa na uwezo wa kutengeneza mitaji”capital formation”,hivyo kupelekea uwezo na uwekezaji hafifu”low investments” na baadae kuwepo kwa kitu kinaitwa “low production”.Profesa Nurke anaamini kuwa umasikini wetu ndio uanzia hapo!

Utitiri huu wa tozo na kodi Nchini ni wazi kuwa unaongeza au utaongeza umasikini Nchini!Natoa rai kwa wasomi Nchini kwenda kufanya tafiti ya jinsi gani ongezeko la tozo na kodi mbalimbali katika mwaka wa fedha 2021/2022 limeweza kupunguza juhudi za kuondoa umasikini kwa watu wa chini!

Mwandishi ni Kijana wa CCM,Makamu Rais wa zamani Serikali ya Wanafunzi Daruso-IJMC,Ofisa wa zamani Idara ya Habari- Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %