0 0
Read Time:1 Minute, 3 Second

Na Hassan Nganzo

Norway

Akichangia hoja ndani Jamvi la Diaspora Dunia , Ndugu Hassan ambae ni mmoja wa waanzilishi wa TDC Global, Taasisi ya Watanzania waishio ughaibuni alisema..

Kwa ufupi tu ni kwamba Serikali ilisha bainisha toka hapo awali kuwa wanampango wa kutoa Hadhi Maalumu ambayo kwa sasa imeshafikia hatua za mwisho na kwa upande wa Zanzibar ilisha kamilika toka mwaka jana.
Kuliongelea neno Uraia pacha ni jambo la kawaida kwani watu wengi ndo limewakaa kichani kuliko hili la hadhi maalumu ambalo ndilo tegemeo halisi lijalo.
Kwahiyo ni vema kwa wanadiaspora kuendelea kutambua kuwa tunasubiri Hadhi maalumu na kuepuka kuingia katika mawazo ambayo hayapo.
Mh Waziri kaliongelea kwa jina la Uraia pacha huwenda ni kwa sababu ya maongezi yaliyokuwa yakifanyika katika mkutano wake na waandishi wa habari lakini jibu kamili lipo wazi na nimeambatanisha Clip za viongozi mbalimbali wakifafanua maswala ya Hadhi maalumu.

Na pia ijulikane wazi kuwa nchi nyingi zenye uraia pacha utakuta kuna vitu vingine vimezuiliwa katika uraia pacha huo,kwahiyo jina uraia pacha unakuwa hauna maana yoyote kwa kuwa na vikwazo kwa mambo kadhaa.
Kwa kifupi huo sio urai pacha bali ni HADHI MAALUMU.
Hadhi Maalumu ni utambulisho rasmi ambao unakufanya uweze kuwa na makubaliano kadhaa ambayo yatakupa fursa ktk nchi yako.Nchi nyingi wameondoa kuwepo na kujihusisha kisiasa.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %