0 0
Read Time:4 Minute, 40 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya!
Desemba 4,2021.

Ni mwaka jana tu, kijana na kada wa Chadema ndugu Godbless Mallisa alikuwa amepewa kazi maalum na Chama chake ya kutaka kuwatisha watanzania kupitia kivuli cha Bunge la Ulaya kwamba muda si mrefu Nchi ya Tanzania ilikuwa inakwenda kuwekewa vikwazo na jumuiya ya Ulaya!Mpaka leo, hakuna kikwazo na wapo kimya!

Mipango yao dhaifu Chadema kwa sasa inajengwa katika mbinu ya kutafuta huruma huko barani Ulaya kupitia Makamu Mwenyekiti wa Chama chao Ndugu Tundu Antipas Lissu, ambaye amekuwa akitumika na Chama chake kufanya mambo makubwa mawili kuhusu Tanzania ambayo ni “demonisation & disinformation about Tanzania”.

Mpango huu mahususi na maalum wa Chadema umekuja ukiwa na malengo mkakati makubwa mawili;Kwanza(i)kuhakikisha kuwa iwe kwa gharama yoyote ile,wanaweza kumuokoa Mwenyekiti wao Chama Taifa,Mh. Freeman Mbowe dhidi ya mikono ya sheria(ii)Pia wanataka kuhakikisha kuwa,ule mpango wao wakati wa Serikali ya awamu ya tano kuhusu Tanzania unaendelea”demonisation”kwa lengo la kuendelea kupata ruzuku ya kuendesha Chama toka vyama rafiki vya nje,njaa ni kali pale kinondoni kwa sasa!

Kwa watu tunafwatilia siasa za Bunge la Ulaya hasa mjadala mzima na sio vipande vipande vinavyosambazwa kimkakati na Chadema kupitia mitandaoni, hatuwezi kustuka na uhuni huu.

Mjadala wa kikao cha kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya, kilipitia kitu kinachoitwa “Tanzania situation”, kitu ambacho pia ufanyika kwa Nchi kadha washirika wa jumuiya ya Ulaya!Huu ni utamaduni wao wa kila mwaka, Balozi Rita Laranjinha ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ulaya,akitanguliwa na utangulizi wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, David James McAllister ambaye wote mnamjua anatoka Chama mshirika wa Chadema pale Nchini Ujerumani!

Baada ya mada ya Balozi Rita Laranjinha,alifwatiwa na msaidizi wake, aliyejikita katika kuwasilisha kuhusu hali ya ushirikiano wa kiuchumi baina ya Nchi ya Tanzania na Ulaya, baadae kufwatiwa na michango ya wabunge na baadae Mwenyekiti McAllister akahitimisha!

HAYA NDIO MAUDHUI MAKUU YA KIKAO HICHO NA SI VINGINEVYO.

1.Nipende kuwatoa hofu watanzania kwamba,Nchi yetu ya Tanzania haikujadiliwa mahali popote na Bunge la jumuiya ya Ulaya na kuazimiwa na baadae kuazimiwa na Bunge zima la jumuiya ya Ulaya, kama ambavyo imekuwa ikipotoshwa”disinformation” na baadhi ya watu.

Kwa ufupi,mpaka dakika hii,hakuna azimio lolote na popote la Bunge la Jumuiya ya Ulaya kuhusu hali ya kisiasa na haki za binadamu Nchini Tanzania,hakuna.

2.Balozi Rita na msaidizi wake,kwa umahiri mkubwa walijaribu kufanya uwasilishaji wa mada zao kitaalam zaidi kwa takwimu na uwazi mkubwa ambazo zilitoa nafasi za kuwasilisha “views” za pande zote zilizozungumziwa kikaoni”balanced”.

3.Pamoja na wawasilishaji mada kuzungumza mambo chanya na hasi “challanges & Opportunities”,pia mada zao zilitambua umuhimu wa Nchi ya Tanzania katika kuendeleza ushirikiano kati yake na jumuiya ya Ulaya na wakakiri kuwa, Nchi ya Tanzania ni moja wa washirika wa kimkakati wa jumuiya ya Ulaya katika masuala mengi ya kimkakati!

4.Kama ilivyo kwenye vikao vya Bunge la Ulaya vya kila mwaka,hata kile kikao cha mwaka jana,wabunge waliojadili hoja kuhusu Tanzania, hawakuzidi angalau hata wabunge sita, kati ya Bunge lenye wabunge takribani sabini na moja wa Bunge zima la Jumuiya ya hiyo.Katika mukutadha huo ni uzushi kusema kuwa, wabunge watano wanaweza kufanya maazimio na hii inakupa picha kuwa ule ulikuwa mjadala wa changamsha Bunge!

5.Kama ilivyo kawaida yake, mshirika namba moja wa Chadema barani Ulaya ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ndugu McAllister,bado alitaka kuendeleza propaganda alizozitengeneza kwenye kikao cha November 2020 kwa kutaka kuionesha dunia kuwa, hali ya siasa Nchini Tanzania ni mbaya na kutaka kuliaminisha Bunge la Ulaya kuwa wanachama na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini Tanzania wanakumbana na uvunjifu wa haki zao za kidemokrasia pamoja na matukio ya kushikiliwa na dola kinyume cha sheria na kupewa kesi za kisiasa!

Kinyume chake,Mh Balozi Rita, alisema kuwa kuna,kwa sasa kuna matumaini makubwa Nchini Tanzania,chini ya Uongozi wa Mh. Rais Suluhu Samia Hassan hivyo jumuiya hiyo kuipongeza Nchi ya Tanzania kwa mafanikio hayo!

Aidha Balozi Rita aliendelea kuimwagia sifa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Samia Hassan,kwa kuendelea kujali masuala ya uhuru wa maoni,uhuru wa vyombo vya habari, ambapo alisema kwamba mabadiliko hayo yamepokelewa vyema kitaifa na kimataifa, japo alidai kuwa bado kuna baadhi ya sheria zinazolalamikiwa katika eneo hili ambazo anaamini zitashughulikiwa!

MWENYEKITI McALLISTER NDIO “PUNDA” WA CHADEMA KATIKA KUICHAFUA TANZANIA BARANI ULAYA!

Mwenyekiti wa Kamati ya mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya, Ndugu yangu McAllister, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Ulaya tokea Chama cha CDU cha Nchini Ujerumani, ambacho ndio chama mshirika namba moja wa Chadema Ulaya kwa sasa kikibeba jumuiya ya muunganiko wa vyama duniani,ameendelea na mpango wake wa KUICHAFUA Tanzania kupitia Tundu Antipas Lissu.

Kabla ya Ndugu yangu McAllister kuhudhuria kikao kama hiki mwaka Jana,Hapo kabla aliweza kuonana kwanza na Ndugu yangu Tundu Antipas Lissu, ambaye alitumika “kumpanga” mbunge hiyo kwa ajili ya kutimiza malengo yao ya kisiasa!Kwa kuthibitisha hilo,Kijana wa Chadema Ndugu Godbless Malissa alitumika sana kwenye mitandao ya kijamii kutaka “kuboost” ajenda hiyo japo baadae ilikwama vibaya!

Katika akili ile ile,chombo kile kile na “PUNDA” yule yule,this time, Chadema wanataka tena watumie Bunge la Ulaya kwa ajili ya kuitisha serikali ya CCM na mahakama na hatimaye kuweza kumchomoa Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Mbowe na wenzake, mbele ya mkono wa sheria!

Serikali ya CCM chini ya Mh.Rais Samia Suluhu Hassan haiwezi kuyumbishwa na propaganda hizi za Chadema LAKINI pia watanzania ni kama wameshajua janja ya Chadema na sasa ni kama wanawacheka,eti wanasema,SABAYA Je?

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %