0 0
Read Time:44 Second

WU®

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa kuzingatia haki na uadilifu kwa kutambua dhima kubwa waliyonayo kwa Mwenyezi Mungu.
 
Alhaj Dk Mwinyi amesema hayo kwa waumini wa Dini ya kiislamu baada ya kukamilika kwa sala ya Ijumaa iliofanyika Masjid Al – Qudus uliopo Kijitoupele Jijini Zanzibar.
 
Alisema watumishi wa  umma wana wajibu wa kufanya kazi  kwa kuzingatia uadilifu na kutambua nafasi walizokabidhiwa ni dhima kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo wanapaswa kufanya haki na kuondokana na dhulma.
 
Aliwataka watumishi hao kuondokana na dhana iliojengeka miongoni mwao kuwa mali ya Serikali haina mwenyewe.
 
Alisema Serikali inahitaji fedha kwa ajili ya kuendeleza kazi za maendeleo, hivyo akatowa wito kwa wafanyakazi wa Serikali pamoja na wafanyabiashara kuwa waadilifu, hususan katika suala la ulipaji wa kodi.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %