0 0
Read Time:51 Second

WU® Media PRODUCTION

Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe.Mahmoud Thabit Kombo amekutana na wawekezaji wakubwa Wakiitaliano wanaowekeza katika Sekta ya Utalii nchini Tanzania ikiwemo visiwani Zanzibar pamoja na Jumuiya zao zote za Uwekezaji katika Sekta ya Utalii, Wamiliki wa Hoteli mbali mbali zilizopo Zanzibar na Tanzania Bara wanaotokea Italia pamoja na hao pia amekutana na Wamiliki wa Mashirika ya Ndege ya Misafara Mirefu ya Watalii (Long Haul Flights ya Neos na Blue Panorama,ambao wameanza kutayarisha Misafara yao Mikubwa ya Watalii kwenda Zanzibar na Tanzania Bara baada ya masharti ya Janga la Uviko kuwa nafuu.

Mhe. Balozi Kombo alikutana na Jumuiya hiyo ya ASTOI pamoja na Rais wao na wanajumuiya wote ambao wamerudhishwa na maelezo ya Balozi na kukubali kuanza misafara yao hiyo hivi karibuni baada ya kufuatilia maelezo na Hotuba za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na kikao cha Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui alichofanya na Mhe. Balozi pamoja na wawekezaji hao, akiwepo Balozi wa Italia nchini.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %