
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
March 6,2022.
Wajibu wa Chama cha siasa makini duniani kote lazima uwe ni wazo zaidi ya kushika na kuiongoza Serikali au dola,Chama ambacho kimeweka akili na ndoto zake katika kushika dola pekee yake kwangu naweza kukiita ni Chama dhaifu kiitikadi na kifalsafa!Kushika dola pekee hakuwezi kukufanya uwe Chama kinachoweza kuaminika mbele ya Wananchi miaka nenda rudi!Otherwise you opt to be a tempory au seasonal Opposition Party!
Chama makini cha upinzani lazima kiwaze na kijenge malengo mengine ya zaida ambayo yana maslahi mapana kwa Taifa na watu wake wote nje ya Itikadi zao!
Dola ushikwa na mara NYINGINE upotezwa na vyama na mifano ipo mingi Afrika HII!KANU ya kenya imewahi kupoteza Dola na mifano mengine mengi afrika hii!
Ni rahisi sana kushika dola lakini pia ni rahisi sana kupoteza dola endapo Chama cha siasa kitakosa maono, mawazo na Itikadi pana ya kuisimamia huku lengo la kushika dola likienda sambamba na malengo mengine makuu!
Kuna msemo katika siasa na katika State vs Powers unasema”Absolute Powers collapse Absolutely”!Njia pekee ya Chama Cha siasa kuweza kuwa na radhaa Kwa watu ni kusimamia misingi mingine ya KITAIFA!
Misingi hii kwa mfano hapa kwetu Nchini Tanzania ni pamoja (I)UMOJA na mshikamano wa KITAIFA(II) Uzalendo kwa Taifa lako bila kujali Itikadi Yako(III)Kuweka MBELE maslahi mapana ya Tanzania hata kama yanakwaza malengo ya Chama chako ya kuchukua Dola!Chama Cha namna hii kinaweza kuishi milele katika siasa!
Kwanini KANU ya Kenya imeanguka lakini CCM ya Mwalimu Nyerere inadunda Tanzania na inaendelea kupeta?
Jibu langu ni rahisi sana!Sio kwamba CCM kama chama hawafanyi makosa flani flani ya kisiasa zaidi ni kwamba CCM ndio Chama pekee katika Afrika ambacho misingi yake inabebwa na nguzo kuu tatu(I)UMOJA wa kitaifa(III)Uzalendo na (Amani & udugu).Wakati KANU ya Kenya ilijikita katika ukabila CCM iliwahi mapema kuukata ukabila!Unategemea CCM usiaminiwe?
CDM NA WAPINZANI WENGINE WATOKE VIPI KUANZIA SASA?
1.Lazima wapinzani wapanue wigo wao na malengo yao yasiwe katika kuchukua dola tu,hasara za kuiwaza dola na kuwaza kunyakua majimbo tu wakati wa uchaguzi ndio upelekea wanasiasa kukosa uvumilivu”Political torelance”na kuwaza mabaya dhidi ya NCHI zao!
2.Lazima Chama makini cha upinzani pia kiwaze katika kujenga Vijana wenye ushawishi na uwezo ndani ya Taifa!Ukishajenga Vijana wazalendo na wenye uwezo mkubwa kuna siku Chama chako kitaaminiwa tu na wananchi,inabaki kuwa suala la muda!
3.Chama imara cha upinzani lazima kije na miradi yake ya mfano”case studies” Ili watu wakiona mifano hiyo waweze kujiamini Chama husika!Hivi ACT wazalendo au CUF,au CDM wana nini cha kuwaonyesha”show casing” Watanzania kwamba “they also can do?”
Miradi hiyo ya kimkakati inaweza ikawa ni miradi ya kisiasa,kiuchumi au kijamii!Angalia wenzenu CCM wameshajenga Chuo cha Itikadi na uongozi pale kibaha Pwani japo Kwa ushirikino na vyama vingine Afrika lakini CDM mpaka leo wapo kinondoni kwenye kijumba kidogo kama ofisi kuu!Nani atawaamini?
4.Je,wakati wa Uchaguzi wapinzani wanahubiri nini?Amani na upendo au Shari na kuandamana?Nani atakuheshimu kwa maono hayo?
Mawazo ya kutaka kushika dola iwe isiwe ndio uleta kifo kwa Chama kikubwa kama CDM!”Absolute Powers Collapse Absolutely” ndio hiyo!
Niliwahi kuandika kuwa wanajeshi kabla ya kuingiza askari wake vitani lazima wafanye kitu kinaitwa”APPRECIATION”.Katika kufanya appreciation wanaangalia vitu vingi vya msingi kabla ya kuingiza askari katika uwanja wa medani!
Huu ni wakati sahihi sana wa CDM sasa kufanya “appreciation of the political ground”kabla ya kukurupuka kuanza upya mipango ya kuitafuta dola upya mwaka 2025.
Commitment ya Mwenyekiti Mbowe kwa Mh. Rais Samia inaweza isiwe na maana yoyote bila kufanya kitu ambacho majeshi na makamanda wao wanakiita “ground appreciation”.Uchawi wa ushindi wa vita vyovyote duniani, pamoja na mambo mengine, upo katika ground appreciation!
CDM kama wanataka kuwa Chama tishio leo na kesho cha upinzani Tanzania na Afrika basi wanapaswa kufanya”quick appreciation” katika maeneo ya Itikadi Yao,Maono Yao,Mbinu zao na hata kwenye political strategists wao ni watu gani?
Mwenyekiti Mzee wangu Freeman Mbowe una nafasi ya kukifanya Chama hiki kuwa kikubwa na kukipa heshima Afrika na hiyo ndio itakuwa “positive legacy” yako kwa watanzania na wana CDM pia!
+255784159968.