1 0
Read Time:2 Minute, 2 Second

Na KNM

WUยฎMedia PRODUCTION

Balozi wa Tanzania nchini Italia siku ya jumapili ya tarehe 06/0/2022, amekutana na Watanzania mjini Rome,kutoka mikoa mbalimbali ya Italy. Mkutano huo uliofanyika katika ubalozi wa Tanzania Rome pia ulihudhuriwa na Mhasham Baba Askofu ambae pia alipata nafasi ya kutoa nasaha zake ambazo aliweka msisitizo katika kuimarisha umoja na upendo baina ya Watanzania.

Mkutano huo ulioanza saa nne asubuhi na kumalizika saa kumi na moja jioni kwa mpango kazi uliohitimishwa na Mh Balozi. Balozi kama mlezi alipata nafasi ya kusikiliza changamoto za jumuiya za watanzania wote Italy na kwa njia moja au njingine kuzipatia ufumbuzi wa papo kwa papo.

Mkutano huo ambao ulikuwa ni wa kwanza kufanyika wa aina yake baina ya diaspora na Mh.Balozi tangu afike kuchukua majukumu yake mapya miezi takriban mitano sasa, Wana diaspora walipata fursa kubwa ya kujua majukumu ya balozi na ubalozi ambayo yaliainishwa vyema na Mh. Balozi Mahmoud Thabit Kombo. Diaspora pia walipata kujua fursa mbalimbali za kuwekeza na biashara nchini Tanzania, ambapo kupitia maofisa wa ubalozi ambao kila mmoja ana majukumu tofauti wataweza kuwasiliana nao moja kwa moja kufikia adhima yao ya kuwekeza au biashara katika sekta mbalimbali.

Katika mkutano huo Viongozi wa diaspora walitoa pongezi nyingi kwa Mh Balozi kwa kuweza kuandaa mkutano huo ambao kwao ulikuwa na faraja kubwa, diaspora walimpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua balozi Mahmoud Thabit Kombo ambae tangu amekuja amerudisha hari na nguvu mpya kwa jumuiya za diaspora Italy. vilevile kulikuwa na kipindi cha maswali yaliyoulizwa na watanzania na baadae kujibiwa kwa majawabu na Mh. Balozi.

Katika mpango kazi Mh Balozi ametangaza ratiba maalumu ya kukutana na makundi ya diaspora kwa mwaka mzima. Balozi kama mlezi kwa mamlaka yake ameamua kuirudisha kamati kuu ya diaspora kuendelea na kazi kwa kipindi kingine na kuitaka kamati kupitia mwenyekiti wake Ndugu Kagutta N. Maulidi, kuwa na mkutano na yeye balozi mara moja kila miezi mitatu yaani mara nne kwa mwaka.

Mkutano uliendeshwa kwa umahiri mkubwa na (HOC) Mkuu wa utawala wa ubalozi Bi Jubilata E. Shao ambae kwa ridhaa ya Mh. Balozi alifunga mkutano kwa kuwashukuru sana diaspora kwa mahudhurio makubwa na kuwatakia safari njema wanaporejea makwao.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Genova kwa niaba ya Jumuiya yao amzawadia Mh Balozi,mama Balozi na Bi Jubilata E.Shao, kwenye mkutano uliowakutanisha Diaspora Italy na Balozi wa Tanzania Italy Mh. Mahmoud Thabit Kombo.

Happy
Happy
100 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %