WU®Media PRODUCTION
WAZIRI AWAPONGEZA DIASPORA WA HUNGARY
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Africa mashariki Mh. Mulamula ameongea kuhusu Hali ya usalama wa Watanzania nchini Ukraine kufuatia kuzuka kwa vita Kati yake na Urusi.Waziri ameuhakikishia UMMA wa Watanzania kuwa ndugu ,jamaa na wazazi wa wanafunzi na Watanzania kwa ujumla walioko Ukraine kuwa wapo salama Pamoja na changamoto za kiusalama, Serikali imekwisha fanya Mawasiliano na pande zote ili kuhakikisha Watanzania wanapata msaada na ulinzi kuweza kufika Moscow.
Waziri amewapongeza Diaspora wa Tanzania nchini Hungary kwa kuwa mstari wa mbele kutoa msaada kwa Watanzania wanaokimbia Ukraine na kuingia Hungary.