WU® Media PRODUCTION
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 8 Machi akishiriki Jukwaa la Uchumi Duniani kwa Kanda ya Afrika lililofanyika kwa njia ya mtandao. Makamu wa Rais amekuwa mgeni rasmi katika majadiliano hayo yalioshirikisha viongozi mbalimbali wa serikali ,sekta binafsi na mashirika ya kimataifa kutoka nchi za ukanda wa Afrika katika mada iliojadili namna teknolojia inavyoweza kutumika katika kukuza biashara ndogondogo na za kati ili kuchangia uchumi kwa nchi za Afrika baada ya athari za Uviko 19.