0 0
Read Time:2 Minute, 15 Second
JICHO LA ULEDI

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
March 18,2022.

Juzi nimemsikia RAIS na Mama yangu kipenzi Samia Suluhu Hassan wakati akihojiwa na DK Ayub Lioba pale TBC I.Mama anasema anafikilia kubinafsisha Bandari ya Dar Ili kuongeza mapato zaidi na anasema inawezekana baada ya ubia Bandari ya Dar inaweza ikatengeneza robo ya Bajeti yetu yote ya mwaka!

Nilistuka KIDOGO!Nilitarajia Dk Lioba angestuka na kumuuliwa Mh.Rais swali zito au kutaka ufafanuzi zaidi kwani inawezekana Mh.Rais labda ana points zaidi ya tunavyowaza sisi!

Ukubwa wa Nchi fulani sometimes upimwa kwenye maono ya watawala wake !Mfano mzuri, ukimsikia maono ya RAIS wa China XI Jin Ping wapi anataka kuipeleka China”make the China great again” unaweza kuona jinsi ramani ya China ya kuitawala Dunia kupitia majini”Bandari” ilivyochorwa na kutekelezwa kiufundi kuelekea kutawala dunia kupitia Bahari!

Wakati Rais XI Jin Ping wa Uchina anawaza kutekeleza mpango mkakati wa kiuchumi,kiulinzi na kisiasa wa China dhidi ya Afrika kupitia kitu kinaitwa “Belt & Road Initiative”,RAIS na Mama yangu kipenzi anawaza kuingia ubia wa kuendesha BANDARI ya Dar!Mama anatakiwa anikalishe darasani asichoke!Bado sijaelewa!

Namnukuu mchumi mmoja wa China anasema,”Belt & Road initiatives forges political,economic & security tie between China and Africa inorder to advance geopolitical interests of Beijing..”

Tunawezaje kuwa Taifa kubwa kama tunashindwa kumanage mambo madogo madogo baada ya miaka 60 ya uhuru wetu?Otherwise tuambiane kuwa hatuna tena ndoto zile tulizokuwa nazo wakati wa hayati JPM ya kutufanya kuwa Taifa kubwa na Taifa tajiri kupitia geographical competitive advantage yetu.

Ilani yetu ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 mpaka 2025 pamoja na mambo mengine,inatutaka na kutuelekeza kutumia vizuri jiographia yetu kama Nchi pamoja na bahari yetu ili kutufanya kuwa watawala wa BIASHARA majini na aridhini ndani ya ukanda wa Afrika mashariki na kati.

Wakati watanzania wengi tunawaza jinsi gani ya kutanua BANDARI ya Bagamoyo kwa fedha yetu hivyo kujiongezea wa mapato na kuifanya SGR na TAZARA kuweza kuchochea BIASHARA na majirani zetu,leo tumeanza kuwaza ubia katika eneo nyeti la BANDARI?

Kuingia ubia inawezekana kukaweza kuongeza mapato ya Bandari ya Dar es salaam lakini Je,hatuoni kuwa mapato hayo tunaenda kugawana na mbia wetu?Ni KWELI tutakuwa tumeongeza mapato lakini mapato hayo hayo tunaenda kugawana na mbia!Biashara ya wapi hii?

Hivi direction yetu kama Nchi ni ipi?tunataka kuachieve nini?tumefika wakati tunataka kuuza “Ukubwa Wetu” sababu ya fedha?tumeshindwa kujua sisi ni nani?

Mama yangu na serikali yangu ya CCM anapaswa kushauriwa vizuri zaidi ya ushauri huu wa kuingia ubia katika Bandari ya Dar es salaam!Yaani tumekosa vijana wa kitanzania wenye weledi wa kuendesha BANDARI kwa faida?!KWELI tunataka kusurender Usalama wa majini wa Taifa letu kwa wageni?

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %