Mwandishi huru :
Mathayo Samson Kizinga
+255718 932888
kizinga05@gmail.com
Si tu Dr John Pombe Magufuli alikuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania ndio maana watu wanamkubuka, lahasha! Bali ni Rais wa kipekee Sana kati ya awamu tano zilizopita.Upekee wake unatokana na kipaji cha kipekee alichojaliwa na Mwenyezi Mungu cha uwezo wa kupenda vitu vizuri,kubuni na kufanya vitu ambavyo vinaakisi Tanzania ya Sasa na vizazi vijavyo.John Pombe Magufuli ni adhama ya kipekee.
Rais Nyerere na Rais Mkapa walizikwa na wanakumbukwa kwa mambo mazuri ila Rais John Pombe Magufuli alizikwa kipekee na anakumbukwa kwa mambo yake mazuri ya kipekee.Tekodi za mtandao kwa picha na maandishi zinaweza kuthibitisha haya.
Kwanini John Pombe Magufuli ni tunu na adhama ya kipekee? Hii ni kutokana na ukweli kwamba uzalendo wake ulikuwa wa hali ya juu Sana.
Mosi , Uwezo wa kizalendo wa Dr John Pombe Magufuli unajidhihirisha kuutokana na hatua za maendeleo aliyoaacha kwa kwa kuingoza Tanzania kwa muda mfupi.
Pili , Uwezo wake wa kipekee kuthamini utu na hivyo kujali huduma bora zitolewe katika haki , wakati muafaka na kwa ubora unaostahili binadamu bila kiongozi au mfanyakazi kuutweza utu.
Tatu , uzalendo wake wa dhati kulinda dafina za nchi ya Tanzania dhidi ya nchi za ughaibuni.Alikuwa vizuri Sana katika intelijensia ya uchumi.Ni mtu wa kipekee Sana asiyehofu, makini ambaye hawezi kuingizwa mkenge katika makubaliano au mikataba ya uchumi.Hii na nyingine ni sababu mojawapo amekuwa mashuhuri Afrika na dunia nzima kama walivvyokuwa Marais wa Afrika wapigania uhuru miaka ya 1950 – 1970.Kifo chake kinaombolezwa dunia Zima na huu ni upekee tofauti na Marais wengine walioaga dunia.
Watu wengine wanamwita hakuwa mwanasiasa mzuri au mwanadiplomasia mzuri.Hasa kutokana Imani potofu na ukweli kwamba eti mwanadiplomasia mzuri lazima atembee Sana ughaibuni au apendwe Sana na mataifa ya ya kibeberu .
Nasema hii ni imani potofu sana kwasababu nje ya nchi kuna balozi, Rais Magufuli kwa uzalendo wake alipunguza matumizi mabaya ya fedha za umma, na kwa msimamo na uzalendo wake asingeenda kichwa kichwa ughaibuni.Hebu tujiulize ni Mara ngapi Rais wa Marekani au nchi za Ulaya na Asia kama China unasikia Marais wao wapo ziarani nje ya mataifa yao?Ukweli wanatoka kwa nadra Kama alivyokuwa John Pombe Magufuli.
Nne. John Pombe Magufuli alipigania utamaduni wa Kiswahili. Si tu kuhakikisha Kiswahili kimeenea kwa haraka na kasi na kutumika ughaibuni kama lugha adhimu .Bali alipenda kuongea Kiswahili kuliko Kiingereza .Mfikirie Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au mtangazaji anayechanyanya maneno ya Kiingereza katika Kiswahili anapo ongea kila sentesi na anasikilizwa na wanakijiji wengi wasiojua utamaduni wa Kiingereza. Inakuonesha alivyo mtumwa wa fikra na matendo, yupo Tanzania ila Kisaikolojia anaishi Kizungu.Je, amesoma na kupata ukombozi wa kifikra?
Ukweli ni kwamba Wazungu wanapendelea kututumia sisi, kutuaminisha hatuwezi bila wao, ndio maana wasomi wetu wanaamini ujumbe hauwezi kufika bila maneno ya Kiingereza katika kila sentesi.Huu ni utumwa wa wasomi wetu kifikra Imani na matendo.Watu ambao wanatakiwa wawakomboe wasio na Elimu rasmi ndio wanatakiwa wakombolewe. Hawana Uwezo wa kuona vizazi vijavyo wataishi namna gani kama alivyochakata na kubangua bongo kwa upendo mkubwa wa nchi hii John Pombe Magufuli.
Tano. Maono ya Mbele kwa ajili ya vizazi vijavyo.Ukweli ni kwamba Dr John Pombe Magufuli alichukiwa Sana na baadhi ya wasomi na wafanyabiashara wakubwa na haramu.Sababu kubwa ni ukweli kwamba alipishana nao maono.Wakati wao wakiwa wameamini katika nadharia za Kimagharibi ,yeye aliona hayo ni machweo ya bara la Afrika.Mfano kuamini unyonyaji, biashara haramu,uonevu, lugha ya Kiingereza na kuwamini Wazungu kupita kiasi.Yeye alikuwa na mrengo wa Mashariki kiasi na Afrika Mashariki zaidi kwamba hayo ni mawio ya kuangaza Sasa na watoto wetu wanaovuvumka kuiheshimu Lugha yetu, Elimu yetu, dafina zetu , Teknolojia yetu,viwanda na uewezo wetu binafsi.
Wakati yeye akiamini kitaifisha ili kila mtu apate unafuu wasomi na wafanyabiashara haramu waliamini kujibinafsisha na kutumia watu wengine vibaya kwa maslahi binafsi.Hawa ndio waliokuwa maadui wakubwa wa John Pombe Magufuli wakimsema vibaya kwa chuki na propaganda .
Ni ukweli usio na kifani kuwa John Pombe Magufuli ndiye Rais anayependwa zaidi na wananchi na fikra zake zinaishi zaidi baada ya Nyerere kwani wengi wanaoishi Sasa walimwona zaidi John Pombe Magufuli na wanamsikia tu Nyerere.
Huu ndio ukweli kwamba alipishana watu haramu ,wabinafsi na watumwa wa lugha ya Kiingereza na utamaduni wa Kiingereza.Unaposoma kila kitu kwa Kingereza ni ukweli usiopingika unafundishwa kuthamini utamaduni wa Kiingereza, fikra za Waingereza, imani na maendeleo ya Waingereza.
John Pombe Magufuli alikuwa anatukomboa ila ilikuwa ngumu kwa kundi hili la watu walioishi kimwili tu Afrika na Kisaikolojia ughaibuni.Watu hawa si tu walituangusha Sana na wanatuangusha Sana kupiga hatua za maendeleo ya Sasa na vizazi vijavyo.
Hawa ni watu wanaosoma makaratasi, wanatafiti makaratasi, wanatunukiwa makaratasi,wanathamini makaratasi, wanaaandika makaratasi hawavumbui vitu vinavyoonekana wanavumbua makaratasi.
Rushwa Rais Magufuli alidhibiti sana mianya ya rushwa na biashara haramu Mfano . Utakatishaji fedha, madawa ya kulevya, wafanya kazi hewa, usafirishaji wa binadamu, madanguro, matumizi mabaya ya ofisi za serikali na mikataba ya ovyo.
SASA tuna Rais mwingine Mama Jemedari, Nguli wa Siasa muda mrefu na mtulivu mkubwa wa fikra, Samia Suluhu Hassan.
Kwanza amehidi kufuata nyayo za Rais Magufuli kwasasabu moja kuu, waliokuwa bega kwa bega katika kampeni na kuliongoza taifa kutekeleza ilani ya CCM, ukweli walitofautiana utashi na kipaji nadhani ndio sababu Rais H.S.Hassan anaonesha uungwana kuukubali Uwezo wa kipekee wa mtangulizi wake.Hii ni faraja kubwa kwa umoja na mshikamano wa taifa, Muungano, amani na utulivu kwani ni tunu za Tanzania.
Mosi ,MAONI yangu ni kwamba Rais anatakiwa kuwa makini kuingizwa mkenge na watumwa wa kifikra, wabinafsi na wafanyabiashara haramu ambao naona ndio kansa ya maendeleo ya taifa letu ambao tiba yake aoiipata John Pombe Magufuli.
Pili , Rais Samia Suluhu Hassan abuni mambo mengine mapya yenye maslahi kama tunavyona Sasa mfano.anatangaza uwazi kiasi cha fedha zinazokwenda serikali za mitaa na namna zinavyotumika kwa malengo na maendeleo yaliyotakiwa.
Tatu: Maridhiamo ya kisiasa Kama tunavyoona Sasa japo asiingizwe mkenge kwenye dhana ya demokrasia kwa “
1.demokrasia halisi ni kukiondoa chama tawala madarakani ” lahasha!
Ama kwamba demokrasia halisi ni
- “Kuruhusu wanasiasa kusema hovyo au kwenda holela popote wanapotaka hata kuutweza tunu kama amani, mshikamano na Muungano wa nchi mbili” lahasha ! Ukweli ni kwamba misingi ya nchi ya Tanzania unatakiwa kuheshimiwa na kila mtu kulindwa kwa jasho na damu
- Nne Makundi ya kisiasa za maslahi binafsi, lazima yadhibitiwe.Utamaduni wa miaka kumi lazima udumishwe.Kauli tata Kama za Spika mstaafu lazima zikomeshwe, mtazamo hasi kuhusu Rais mwanamke lazimu uangamizwe.
Ukweli ni kwamba kikulacho ki nguoni mwako.Watengeneza nasaba za kisasa wapo ndani ya familia.Wamulikwe na wapatiwe tohara au waasiwe kabisa.Haw ndio wanaotumika vibaya Ughaibuni.
Tano .Rais Samia Suluhu Hassan asirithi maadui wa Magufuli wala asikubali kugombanishwa na mtu ambaye hayupo duniani.Hizo ni laana ambazo zitatutafuna Kama taifa.
Sita , Kisasi , Rais Samia Suluhu Hassan asikubali na asiwakumbatie wanaolipiza Kisasi hasa kwa wale waliokuwa madarakani enzi za Magufuli ama wapioonekana kusifiwa na Rais Magufuli.Tutaligawa taifa vipande vingi.Mbegu ya Kisasi huota kila kizazi, huzaa laana.Tazama Rwanda, Congo, Mashariki ya kati na Urusina nduguze.
Watu aliowakirimu Rais Samia Suluhu Hassan wakiendeleza visasi kwa siri kwasababu waliachwa enzi za Magufuli Basi uchaguzi utakuwa mgumu Sana, nchi haitakuwa na mshikamano.Mtazamo uongozi ni kupokezana, na mzuri katika kazi Fulani apewe aendelee au apewe majukumu mengine ndio utamaduni wetu.
Amani, mshikamano na Muungano wa nchi mbili vidumu!Zidumi vikra za John Pombe Magufuli, zidumu fikra za Mwalimu Julius K Nyerere na Sheikh Abeid Abeid Aman Karume.
Mungu Ibariki Tanzania.