0 0
Read Time:3 Minute, 14 Second
JICHO LA ULEDI

George Michael Uledi.
Kyela,MBEYA.
March 17,2022.

Mara zote katika Biblia, Mungu alifanya matendo ya ishara kwa watawala kabla hajaamua kushusha hasira zake dhidi ya tawala zenye kukaidi maagizo yake Ili mpango wake utimie kwa watu wake katika Taifa fulani.

Lakini zaidi Mungu uwapenda watu wabishi na wakaidi ambao hawataki matakwa na mapenzi yake kutimia!Mfalme Farao wa misri alipewa kila ishara ya ukuu wa Mungu juu ya kutaka kuwaachia wana wa Israel kwenda Nchi ya ahadi ya kanani!

Mwishowe ubishi na ukaidi wa Mfalme Farao wa misri ukaishia kupoteza askari wake wote katika bahari ya Shamu!”Red sea”.

Leo tena ukubwa na ushawishi wa kifalsafa na maono wa hayati John Pombe Magufuli kwa watanzania umeweza kujithibitisha bila kuacha chembe ya yoyote”doughts”.Ukubwa huu wa JPM ambao baadhi ya wana CCM wanaukataa,haukataliki ni ujeuri usio na faida kwa CCM!

Nenda kafanye survey ya haraka haraka kuanzia kwenye magroup ya CCM,mitandao yote mikubwa ya kijamii na mpaka mitaani ndio unaweza kujua ukubwa wa hayati JPM.Ubishi wa baadhi ya wanaccm hauwezi kutufikisha popote zaidi ya kutuangamiza!

Urusi waliamua kubadilisha katiba yao angalau mtu mmoja tu aweze kutawala Urusi milele na milele!WATU kama Vlad Putin Rais wa Urusi uja mara moja na kuishi mara moja katika Taifa fulani!

Uchina waliamua kubadilisha katiba yao angalau mtu mmoja aweze kuitawala maisha yake yotee!Watu kama XI Jin Ping Rais wa China, uzaliwa na kuishi mara moja tu katika uhai wa Taifa lolote lile!

Wakati mataifa makubwa na yenye nguvu duniani kama Urusi na uchina, yanaangaika kuchana katiba zao kwa ajili ya kulinda wakina “Magufuli” wao,watu wao wenye maono ya kuwafanya kuwa “watawala wa dunia”, ninyi na baadhi ya wana CCM mnaangaika kumpiga mawe hayati JPM!Shame!

Sababu zenu za kumpiga mawe ni “cheap” mno na hazina maslahi mapana ya Taifa zaidi ya maslahi mapana ya familia zenu na kesho yenu!

Political strategists wa ccm wanapaswa kuwa wawazi katika hili na kumwambia Mama Samia kuwa hatuna namna kwa sasa zaidi ya kutembea na mtu huyu,mzalendo wa kweli,mwana Mapinduzi na mfia NCHI na wananchi wake!

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa Watanzania CHATO katika kumbukizi za Hayati Dr John Pombe Magufuli 17/03/2022

Mimi nitaendelea kumkumbusha Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa,Samia Suluhu hassan kuhusu umuhimu wa kutembea na falsafa za hayati Magufuli,bahati NZURI Mama Samia ni kama anamjua nini watanzania wanakitarajia kutoka kwake!

Katika mahojiano yake ya jana TBC I na Mwalimu wangu Dk Ayub Lioba akijibu swali la kuhusu costody ya fedha za Umma ipoje!Mama anasema;

“….tunachukua hatua dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za Umma,SEMA sipo vocal tu….”!Ni kama mama yangu anajua kuwa being vocal inasaidia kwanza Wananchi wanakuwa wanajua kuwa Serikali inachukua hatua lakini zaidi watumishi wa Umma sehemu zingine wanakuwa waoga kugusa fedha za Umma!

CCM tuna options mbili tu za kuchagua kuelekea mwaka 2025(I)kutembea katika ndoto na maono kubwa ya mzalendo hayati JPM kwani ndio njia pekee ya kuambatana na ndoto za wapiga kura wetu WENGI na kujihakikishia ushindi wa kishindo wa Samia Suluhu Hassan au (II)tujiandae kupambana na upinzani ambao utatoka ndani ya CCM yenyewe kwenye Uchaguzi wa mwaka 2025!

Hesabu zangu ni kama zinaniambia kwamba utekelezaji wa miradi ya kimkakati pekee ilianzishwa na hayati JPM sio assurance ya pekee ya kuweza kutupa ushindi mzuri mwaka 2025 zaidi zaidi itategemea sana jinsi Serikali yako inavyotembea katika MAENEO makuu matatu!

Rais Samia na Mama Janet Magufuli walipozulu KABURI la hayati Dr John Pombe Magufuli 17/03/2022

1.UZALENDO WA VIWANGO VYA JUU WA RAIS NA WATEULE WAKE!

2.MAONO NA NDOTO KUBWA NA ZA WAZI ZA MH RAIS ZA WAPI ANATAKA KUIPELEKA TANZANIA NDANI YA MIAKA YAKE TISA!

3.MH.RAIS SAMIA LAZIMA HAKIKISHA “WAHUNI” HAWAWI SEHEMU YA SERIKALI YAKO.

Waraka huu tunapaswa kuutunza ili kuja kufanya rejeo ifikapo mwaka 2025.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %