0 0
Read Time:47 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amewataka wananchi Mkoani Arusha kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuhifadhi Eneo la Pori Tengefu la Loliondo, Mkoani Arusha.

Mhe. Mongella ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Arusha, amewataka wote wanaopotosha kwa makusudi zoezi la uwekaji alama katika eneo hilo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 1,500 ambalo ni eneo linalopaswa kuhifadhiwa, kuacha kufanya hivyo kwa kuwa lengo la serikali ni kuhifadhi eneo hilo kwa manufaa ya Watanzania na uchumi wa nchi kwa ujumla wake.

Akizungumza katika kikao kazi kuhusu maendeleo ya uhifadhi wa Pori Tengefu la Loliondo, wilayani Karatu, Arusha, Mongella amesema pia kuwa maandalizi ya kuhamisha wananchi kwa hiyari katika eneo la Ngorongoro kuelekea Handeni, Tanga yanaendelea vizuri yote yakiwa na lengo moja la kuhakikisha uhifadhi endelevu katika Hifadhi ya Ngorongoro.

Pascal Shelutete
SAC CC
TANAPA
7.6.2022

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %