WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Mkuu wa Majeshi Nchini ( CDF) Jeneral Venance Salvatory Mabeyo ametoa Zawadi ya KISIMA kimoja cha Maji kwa Ajili ya Wanafunzi na Wananchi na pia ametoa Ahadi ya Tsh. 25,000,000 kwa Ajili ya uendelezaji wa Madarasa.
Ahadi hizo amezitoa Leo katika Shule ya Msingi Venance Mabeyo iliyopo katika Kijiji cha Pachani, Kata ya Michiga Wilaya ya Nanyumbu alipotembelea kusalimia akielekea Mkoa wa Ruvuma.
Shule hiyo ilipewa Jina lake na Wazazi KUTAMBUA mchango wake, ambapo kabla ya Mwaka 2017 ilikuwa inajulikana kama Shule ya Msingi Michiga “B”.
ITAKUMBUKWA kuwa Jeneral Mabeyo alijenga Madarasa 6, Ofisi 1 ya Walimu na Ofisi moja ya Mwalimu Mkuu, Madawati na Samani za Ofisi baada ya kuikuta Shule hiyo ikiwa na Madarasa 2 Tu mwaka 2017.
” Ukisomesha Mtoto, umesomesha Taifa. Kutoka Kanda ya Ziwa mpaka Kanda ya Kusini “
Tunasema ASANTE