0 0
Read Time:1 Minute, 39 Second

Na Zain Hamza
Mwanadiaspora
Washington DC.

HATARI ZA URAIA PACHA

Tahadhari kabla ya hatari!

Serikali ya Tanzania ikikosea tu kutoa uraia pacha hawa majirani wenye shida ya ardhi kwao wataoana na watanzania kama huyu aliye kwenye video, ili wajipatie uraia pacha.

Wakishapata uraia watawaacha. Tena kwa staili ya talaka nginja nginja na jaji kugonga kirungu kwenye meza. Mali zigawanywe nusu kwa nusu.

Kufumba na kufumbua Tanzania itakuwa hajulikani nani mgeni na nani mtanzania. Huko kwao wenzetu ardhi yao wamewaachia wazungu na baadae wakawapa uraia pacha. Mfano hai ni wa pwani ya Malindi.

Vilevile ardhi yao asilimia kubwa inamilikiwa na wanasiasa wao. Hata ardhi ya kuchunga ng’ombe ni mtihani kwao. Tuliona walivyohaha wamasai kuondolewa Loliondo wakaenda kushtaki huko kwao.

Si hao tu mgeni yeyote akija na gea ya kuoa atapata urai pacha, akichukua talaka anabaki na uraia. Hivi ndivyo wanadiaspora wengi wanavyopata uraia nchi za nje.

Kwenye hadhi maalumu hili tatizo halipo (Special Status Supremacy). Asiye mzawa akipata hadhi maalumu kwa kupitia ndoa. Ni bora asitoke kwenye hiyo ndoa. Akipata talaka hadhi maalumu yake itaisha na hana uraia wa Tanzania.

Wale wapenzi wa paspoti mbili za uraia pacha hawafikirii vitu hivi.

Yeyote aliyeko nje, ana mtaji wa kuwekeza nyumbani na ana nia ya kurudi nyumbani hawezi kukubali kushea haki za uraia wa Tanzania na wageni. Ukizingatia vipato vya wanadiaspora ni vidogo ukilinganisha na matajiri watakaochukua uraia pacha.

Hii ina maana kukiwa na uraia pacha, tajiri kama Dangote akioa mtanzania ataweza kupata uraia wa Tanzania na akabaki na uraia wake wa Nigeria. Kwa kupata uraia wa Tanzania hatalipa tena ada na kodi za uwekezaji kupitia TIC kwa sababu atakuwa na haki sawa za umiliki na raia mzawa wa Tanzania. Anaweza kuingiza nchini wafanyakazi kutoka kwao na anaweza kuhamisha faida yote kujengea kwao. Matajiri wa hivi hawahitajiki kuwa wengi kumiliki ardhi na uchumi wa nchi. Hata ishirini wanatosha.

Hadhi maalumu ndio kiunganishi bora cha wazawa wa Tanzania wenye uraia wa nje na Tanzania. Ni muafaka wenye maslahi pande zote mbili na taifa kwa ujumla.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
100 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %