0 0
Read Time:2 Minute, 54 Second

Na Zain WU® MEDIA

Watanzania wanaoishi nje ya nchi, maarufu kama Diaspora wanakadiriwa kuwa Zaidi ya million mbili ambao wametawanyika Duniani katika mabara yote.

Mwandishi ambae ni mwana Diaspora anaeishi nchini MAREKANI amefanya uchambuzi kuona jinsi gani ambavyo mabenki yetu na serikali kwa ujumla wanaweza kufaidika na uwekezaji wa Diaspora.

WANADIASPORA NA UCHUMI WA KWAO

Dola bilioni ni shilingi trilioni 2, bilioni 305, na milioni 843.

  • Wanadiaspora laki moja, kila mmoja akiweka dola elfu 10 katika benki za Tanzania. Benki zitajiongezea mtaji wa dola BILIONI MOJA.

-Wanadiaspora elfu 20, kila mmoja akinunua nyumba ya dola elfu hamsini. NHC itaingiza dola BILIONI MOJA.

-Wanadiaspora laki moja, kila mmoja akinunua bonds elfu 10 za serikali za miaka mitano. Serikali itakuwa imekopeshwa na wanadiaspora wake dola BILIONI MOJA.

-Wanadiaspora laki moja, kila mmoja akilipa interest ya dola elfu 10 kwa mkopo wa miaka 10, benki za Tanzania zitaingiza dola BILIONI MOJA.

-Wanadiaspora 200, kila mmoja akiingia ubia na muwekezaji wa nje mwenye mradi wa dola milioni 5. Tanzania itapata miradi ya dola BILIONI MOJA.

Hayo yote ni nje ya pesa za rejareja zinazotumwa nyumbani(remmitances). Kwa Kenya inasemekana hivi sasa ndio chanzo chao kikubwa cha fedha za kigeni kushinda chai, kahawa, au zao lao lolote la biashara.

Kuna program za muda mfupi za wanadiaspora wenye fani tofauti ikiwemo lugha tofauti za duniani, kufundisha au kufanya kazi nyumbani. Hili linaweza kufanyika hata kwa mitandao. Tanzania inaweza kupata walimu si chini ya elfu 10 kila mwaka. Na wengine wakiwa ni wa kujitolea. Ethiopia tayari wanazo hizi program.

Haya mambo si hadithi za kusadikika. Wanadiaspora wa Ethiopia (Hadhi Maalumu) wamesaidia kujenga kwao bwawa kubwa la umeme kuliko yote Afrika. Na vilevile wanalisimamia shirika la umeme la Ethiopia.

India (Hadhi Maalumu) wanategemea sana utaalamu wa wanadiaspora wao. Na pia wanadiaspora wao wanasimamia benki za biashara za India nje ya India.

Serikali inayowatupa wanadiaspora wake inapoteza manufaa yote haya na zaidi ya hayo. Kuna wanadiaspora wanaoweza kukopa dola zaidi ya laki moja nje ya nchi na kufanyia miradi Tanzania.

Isitoshe pesa zote hizo zitafungua biashara, kilimo, viwanda na ajira kocho kocho kwa watanzania waliopo Tanzania.

Madhara ya uraia pacha kwa nchi tajiri kwa ardhi na maliasili kama Tanzania yanaeleweka.

Kila ilivyo uraia pacha utatoa fursa kwa raia wa nchi za nje kupata uraia pacha na Tanzania kwa kutumia ndoa au vigezo vingine.

Isitoshe kuna raia wazawa wa Tanzania wenye asili ya nchi za kigeni (waasia, waarabu na wazungu). Hawa wengi wao tayari wana uraia wa nje kinyume na sheria. Kuwapa uraia pacha ni kuhalalisha uraia wao wa nje.

Ukiacha usalama wa nchi, matatizo ya kuwapa wageni uraia pacha na Tanzania ni mengi ikiwa ni pamoja na haya;

  1. Watahamishia pesa au faida kwenye mabenki ya kwao.
  2. Kwa uwezo wao kifedha wataendelea zaidi kumiliki uchumi wa nchi. Hii ikiwa ni pamoja na ardhi, madini na mabenki. Hapo kwa jirani mpaka shirika lao la ndege lina hisa za wageni.
  3. Wawekezaji wa kigeni wakipata uraia wa Tanzania hawatalipa tena kodi za uwekezaji kwa kupitia TIC.
  4. Raia wa kigeni watachukua nafasi za kazi. Tanzania tayari ina uhaba wa ajira.
  5. Wageni wataathiri mila, tamaduni zetu ikiwemo kuanguka kwa lugha ya kiswahili.

Hata wanadiaspora wenyewe watajikuta wamefunikwa na raia wa nje wenye uwezo mkubwa kiuchumi katika kupata fursa za kiuchumi na uwekezaji.

Suluhisho lilio bora, win win situation, ni kuwapa wanadiaspora wa Tanzania HADHI MAALUMU. Hii ikimaanisha ni HAKI ZA URAIA KWAO NA VIZAZI VYAO BILA YA USHIRIKI WA KWENYE SIASA ZA TANZANIA.

Kimfaacho mtu chake!

Nawakilisha.(Zain)
EQUITY BANK MDAU NAMBA MOJA WA DIASPORA
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %