
KUMBUKIZI YA KUZALIWA MWANA MAJUMUI WA AFRIKA DR JPM
George Michael Uledi
Kyela, Mbeya.
October 29,2022.
Siku kama ya leo katika ukanda mzuri wa ZIWA victoria,Bibi yangu Suzana Magufuli alikuwa anamleta duniani kijana Mwana Mapinduzi wa kweli wa Afrika,Mzalendo hodari,Mpenda Taifa la Tanzania na watu wake! Leo Nchi ya Tanzania,bara la Afrika na Dunia kwa ujumla, ilibarikiwa kwa kuzaliwa mtoto wa kiume,Chuma,the game changer of Africa,hayati John Pombe Magufuli !

Ni wazi kuwa mapenzi wa vijana wengi hasa wa CCM(Kizazi cha Watia Nia 10,000 Mwaka 2020),Cha kuipenda CCM mpaka leo na hata kuamua kuipambania kwa dhati kabisa, ilikuwa ni mbegu ya Uzalendo iliyopandwa na KOMANDANTI hayati John Pombe Joseph Magufuli!
Kwa upande wangu JPM alikuwa ni kama KOMANDANTI wangu!Je, Komandanti ni nani?Komandanti ni Mkuu wa Chuo cha mafunzo ya kijeshi! Hayati JPM kwangu alikuwa ni Komandanti wa Chuo cha;

I.Uzalendo, Uchapakazi na UADILIFU wa viwango vya pekee katika mambo yenye maslahi ya Taifa na mtu ambaye alinifundisha kuyashinda maslahi yako binafsi na kusimama na maslahi ya Umma!Nani wa kunifundisha tena haya kwa dhati kabisa toka ndani ya moyo wake?Karibu duniani Komandati John Pombe Magufuli!
II.Hayati alinifundisha Somo la uthubutu na Ujeuri wa kuyatafuta maendeleo ya Taifa!Kauli yake ya kwamba anataka kutengeneza Taifa la watoa misaada na sio Taifa la ombaomba always inatembea kichwani mwangu!Huu ulikuwa ni ujeuri wa maendeleo wa viwango vya juu bahati mbaya ujeuri ule ulikwenda nae Chato kaburini!
III.Komandanti hayati John Pombe Magufuli amenifundisha kuwa Taifa bila Mungu hakuna mafanikio ya kweli,Uteuzi bila kumtanguliza Mungu hauwezi kufika mbali na zaidi utekelezaji wa miradi ya maendeleo bila Mungu hauwezi kufika mbali!Mzee yule Chuma Cha Chato kiliweza kulifanya Taifa kuwa na hofu ya Mungu!
IV.Komamdanti John Pombe Magufuli amenifundisha jinsi ya staili ya Uongozi ya “boss type” inalipa haraka katika kusukuma maendeleo ya haraka ya watu wako!JPM angewasikiliza Chadema,labda tusingekuwa na ndege za Taifa mpaka leo,tusingeenda DODOMA mpaka leo na wala tusingekuwa na BWAWA la Umeme la Nyerere wala SGR leo hii!
V.Komandant hayati John Pombe Magufuli alinifundisha kwamba Uzalendo kwa Nchi yako na UADILIFU inalipa sana!Siku moja Mzee wangu Waziri Mkuu mmoja mstaafu alinifikishia salam za dhati kabisa toka kwa mwamba John Pombe Magufuli kuja kwangu!Keanini vijana wengi waliamini katika hayati?
Jibu ni moja tu,kwa hayati uwezo wa mtu wa kuderiver kazi matters alot kuliko kujuana!Angalia jinsi alivyowachomoa vijana wenye uwezo from nowhere to samewhere “Teuzi” zake zilikuwa result oriented ndio maana vijana wengi wenye uwezo waliibuka ndani ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2020.Komandanti amezaliwa leo🤝🤝
Zawadi pekee ya kumpa Komandanti wangu leo ni zawadi ya uzalendo,Uaminifu na utii kwa Taifa langu la Tanzania,utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Mama Samia Suluhu Hassan na utii kwa Chama chake cha Mapinduzi!
Happy birthday Komandanti wangu John Pombe Joseph Magufuli!
Mwandishi ni kada kijana wa CCM, Makamu,Ofisa wa zamani Idara ya Habari-Maelezo, Ofisa Kadeti zamani Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha, Mhadhiri Msaidizi wa zamani Chuo Kikuu cha Saut na Tumaini na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela mwaka 2020.
+255746726484.








