
WU® MEDIA
Columbus Ohio
Watanzania Wamekusanyika kwa Sala (Misa) na Maombi Pamoja na kutoa salaam zao za mwisho kwa Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mwanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi, Babu Sikare maarufu kama Albino Fulani aliyefariki siku ya tarehe 8/02/2023 kama taarifa zilivyopatikana kwenye mitandao
Albino Fulani ambaye amewahi kutamba na nyimbo kadhaa ikiwemo “Nafasi” aliyoshirikiana na Mwana FA, Sugu na Belle 9 amefariki Dunia akiwa Nchini Marekani.
Mipango ya Mazishi inaendelea na yanatarajiwa kufanyika nchini Tanzania mara baada ya taratibu za kusafirisha mwili kukamilika.
Mungu Amrehemu .. Amen

