
“Ameandika balozi Mbelwa Kairuki katika ukurasa wake wa X (Tweeter)”
Kuanzia jana kuna ujumbe mfupi wa video uliozunguka katika mitandao ya kijamii uliorekodiwa na raia wa Uingereza Mwenye Asili ya Tanzania Bi. Martina Farrall, akielezea maisha yake kuwa hatarini huko anapoishi Ireland ya Kaskazini.
Kufuatia ujumbe huo, Ubalozi umewasilisha taarifa ya Bi. Farrall kwa Mamlaka za Uingereza na kuomba hatua za kufuatilia suala hilo zichukuliwe mapema iwezekanavyo ili kuhakikisha usalama wa Bi. Farrall sambamba na kufanyia kazi shutuma alizotoa ili kubaini ukweli wa shutuma hizo na hatua kuchukuliwa.
Aidha, leo tarehe 6 Agosti 2024 Afisa Ubalozi wa Tanzania anakwenda Ireland ya Kaskazini katika mji anapoishi Bi Farrall ili kukutana na Mamlaka zinazohusika kufuatilia suala hilo.








