
Comoro

Taasisi za fedha zinazoshiriki kliniki ya Diaspora ya Watanzania nchini Comoro zimetembelea Benki ya Meck ambayo ni benki kubwa zaidi nchini Comoro
Taasisi hizo ambazo ni CRDB,NMB na TCB wamekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya Meck,Bwana Ahamada Said ambaye amewaeleza uhitaji wa Benki yake kutoa barua za ithibati ya mikopo ( Letters of Credit) kwa wafanyabiashara wa Comoro wanaonunua bidhaa Tanzania na hivyo kuhitaji ushirikiano wa karibu na Benki za Tanzania.
“Wafanyabiashara wa Comoro wananunua bidhaa nyingi nchini Tanzania na hivyo wanahitaji Letters of Credit ili kukamilisha miamala yao na hapa ndio tunawahitaji ninyi bankers wa Tanzania tushirikiane” alisema Mkurugenzi Mtendaji Ahamada ambae alibainisha pia kuwa kwa mwaka benki yake huwezesha takriban Euro Milioni 60 za biashara ya kuku pekee kwa kutoa barua na hivyo fursa na wigo wa ushirikiano ni mkubwa.
Kwa upande wao,Wawakilishi wa Taasisi hizo walieleza utayari wao kusaidia katika eneo hilo.
Wawakilishi hao waliongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu ambaye aliahidi kufuatilia ili kufanikisha hitaji hilo la Benki ya Meck.









