0 0
Read Time:38 Second

New York

Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Amina Mohammed Ofisini kwake Katika Makao Makuu wa Umoja wa Mataifa NewYork. tarehe 01 Mei, 2025.
Mazungumzo hayo yamelenga katika kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na Umoja wa Mataifa lakini pia wamejadiliana masuala mbalimbali ya Maendeleo kwa sekta za kijamii kama afya, elimu na madeni kwa nchi masikini duniani. Rais Mstaafu Kikwete amekutana na Naibu Katibu Mkuu wa UN kwa kofia yake ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Elimu duniani GPE.
Katika mazungumzo hayo Mhe Kikwete amefuatana na Mhe Balozi na Kaimu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Suleiman Haji Suleiman pamoja na maofisa GPE kutoka Makao Makuu Jijini Washington DC.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %