0 0
Read Time:1 Minute, 15 Second

WU®MEDIA

Rimini Italy

Na Kagutta N.Maulidi

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy umeongoza wadau wa sekta ya kilimo na biashara kwenye maonesho makubwa ya kibishara ya na uzalishaji wa mbogamboga na matunda yanayofanyika mjini Rimini nchini Italy.

Ms. Eva Kaluwa
Kaimu mkuu wa Kituo Ubalozi wa Tanzania Italy
Kaimu mkuu wa kituo Ubalozi wa Tanzania nchini Italy akiwa na Muambata Kilimo Ms. Jacqueline Mbuya wakiwa kwenye mazungumzo na wadau

Maonesho ya mwaja huu yaliyofunguliwa leo asubuhi ya tarehe 6/05/2025 yameshikirikisha Bodi ya kahawa Tanzania, Bodi ya korosho,Bodi ya Chai, mamlaka ya TPHPA, Mamlaka ya udhibiti wa nafaka na mazao mchanganyiko na Bank ya CRDB ambao ni wadau wakubwa katika kuwezesha biashara za kimataifa.

Ms Eva Kaluwa kaimu mkuu wa Kituo Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy, amesema ushiriki wa Tanzania katika maonesho haya makubwa ya kimataifa, utafungua fursa pana kwenye sekta ya kilimo,kuboresha uzalishaji na kuongeza thamani ya mazao ya Tanzania katika soko la dunia. Kaimu mkuu wa kituo pia amesema Tanzania itafaidika katika kupata teknolojia itakayosaidia kukuza uchumi wa nchi kwenye sekta ya kilimo kwa kutatua changamoto za uharibifu wa mazao baada ya msimu wa mavuno.

Ubalozi wa Tanzania umeitikia wito wa waziri wa kilimo Mh. Hussein Bashe wa kuutaka ubalozi kushiriki na kuongoza wadau wa sekta ya kilimo katika maonesho haya ya Macfrut 2025 amesema Ms. Jacqueline Mbuya mwambata Kilimo. Ubalozi pamoja na wakurugenzi wa bodi zote wamekutana na wadau mbalimbali waliofurika kwenye Banda la Tanzania.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %