0 0
Read Time:1 Minute, 23 Second

Economic Diplomacy

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Kosovo kuja kuwekeza nchini katika maeno matano ya kimkakati ambayo ni kilimo, madini,teknolojia, uhifadhi wa mazao ya nafaka na utalii.

Mhe. Waziri Kombo ametoa mwaliko huo Juni 3, 2025 jijini Prishtina wakati wa mkutano kati yake na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chemba ya Biashara ya Marekani iliyopo Kosovo pamoja na Wawakilishi kutoka Sekta mbalimbali ikiwemo zile za uzalishaji viwandani, biashara, teknolojia, kilimo, nishati na madini.

Wakati wa mazungumzo hayo Mhe. Waziri Kombo amesema kuwa Tanzania imeendelea kuwa sehemu salama kwa wawekezaji na wafanyabishara kutoka ndani na nje ya nchi huku akizitaja fursa tano muhimu kwa ajili ya ushirikiano na Kosovo ambazo ni kilimo, madini, teknolojia, uhifadhi wa mazao na utalii.

Akizungumzia kuhusu kilimo, amesema Tanzania inayo ardhi ya kutosha yenye rutuba kwa ajili ya wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo matunda kama vile maparachichi, mananasi na mazao mengine kama korosho, chai na kahawa.

Kuhusu madini, Mhe. Waziri Kombo aliwakaribisha wawekezaji hao kuwekeza kwenye uchakataji na uongezaji thamani wa madini ikiwemo madini adimu ya Tanzanite.

Akizungumzia sekta ya utalii, Mhe. Waziri Kombo alisema Tanzania ina lenga kufikia watalii milioni 5 kabla ya kumalizika mwaka huu 2025, hivyo wanahitajika wawekezaji wenye tija hususan kwenye eneo la ujenzi wa hoteli za kitalii na usafirishaji.

Akizumgumzia mazingira ya uwekezaji nchini, Mhe. Waziri Kombo amesema yameendelea kuboreshwa hususan sheria na miundombinu na kwamba masuala mengine yanayohamasisha uwekezaji, biashara na utalii nchini ni Sera ya Mambo ya Nje yenye msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi ambayo imekuwa chachu katika kuwajengea ujasiri wawekezaji kuja nchini.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %