
Gymkhana basketball court

Ms. Eva Nangela amefungua rasmi michezo ya mpira wa kikapu inayodhaminiwa na HSA Apparel. Ufunguzi huo umefanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar Es Salaam
Ms. Eva ambae ni Diaspora anaeishi nchini Italy amekuwa akishiriki kwa karibu sana kwenye sekta ya michezo nchini Tanzania kwa michakato ya kutafuta fursa mbalimbali kwa vijana nchini lakini hata nje ya nchi. Pamoja na Ms. Eva Nangela alikuwepo balozi anaewakilisha kampuni ya HSA Apparel ya Marekani nchini Tanzania ambae pia ni mchezaji wa mpira wa kikapu Tanzania bwana Josephat Peter Sanka. (pichani)

Timu zilizoshiriki katika ball Launch ni ||
1.Mambo basketball team U16
2.Kigamboni basketball team U13
3.Don bosco U 13
4.Ummatched basketball team 18
5.Oratol basketball U 16

Hotuba ya mgeni rasmi Ms. Eva Nangela
Waheshimiwa wageni waalikwa, viongozi wa HSA Apparel, makocha, wachezaji chipukizi, wazazi, wadau wa michezo, mabibi na mabwana,
Habari za mchana,
Leo nimefurahi sana kusimama mbele yenu kama mgeni rasmi katika uzinduzi wa BALL LAUNCH hii muhimu ya HSA Apparel. Kwanza kabisa, napenda kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kukutana mahali hapa tukiwa na afya njema.
Nawashukuru pia waandaaji, HSA Apparel, kwa kunialika katika tukio hili ambalo lina lengo kubwa la kuendeleza vijana kupitia mchezo wa mpira wa kikapu.
Mchezo wa mpira wa kikapu si burudani pekee, bali ni shule ya maisha. Unawafundisha vijana maadili ya mshikamano, nidhamu, ujasiri, na kushirikiana. Kupitia michezo kama hii, tunalea kizazi chenye afya bora, fikra chanya, na ndoto kubwa.
Kwa vijana mlio hapa leo – mna nafasi ya kipekee. Kupitia skills challenge, 3pt challenge, na michezo ya 5×5, mtajifunza si tu ujuzi wa mchezo, bali pia thamani ya kufanya kazi kwa bidii, kutokata tamaa, na kuheshimu muda na wenzenu.
Ndugu wageni,
Tukio la leo linaunganisha wachezaji 50 kutoka makundi mawili ya umri – wale wa miaka 13–16 na wale wa miaka 17–18. Hii inaonyesha wazi dhamira ya HSA Apparel ya kugusa maisha ya vijana tangu wakiwa wadogo hadi wanapoelekea kwenye hatua kubwa ya maisha yao. Hii ni fursa ya kujitengenezea msingi wa baadaye, iwe kitaaluma, kibiashara au katika michezo ya kitaifa na kimataifa.
Aidha, tunaposhuhudia michezo hii leo, tuwaunge mkono vijana wetu. Wazazi na jamii, tuwatie moyo na kuwa sehemu ya safari yao, maana michezo ni ajira, ni afya na ni urithi wa taifa.
Napenda kutoa pongezi kubwa kwa HSA Apparel kwa kuanzisha program kama hizi. Ni mfano bora wa taasisi binafsi kushirikiana na jamii katika kuinua vipaji. Nawasihi muendelee, na sisi sote tuwape msaada ili ndoto za vijana hawa zitimie.
Mwisho, nawakaribisha nyote kufurahia burudani ya michezo itakayofanyika leo – All Stars Game, Top Coaches, na Top Players. Nawaombea vijana wetu kila la heri, na nina imani kuwa kesho kutakuwa na mastaa wakubwa wa kimataifa ambao chanzo chake ni hapa Gymkhana.
Kwa heshima kubwa, natamka rasmi kuwa hafla ya BALL LAUNCH imezinduliwa.
Ahsanteni sana,
Mungu awabariki.











