0 0
Read Time:2 Minute, 37 Second

Na Kagutta NM | 25-4-2025 CASERTA ITALY

DIASPORA BALOZI UNGANANA NA WATANZANIA KUSHEREHEKEA MIAKA 62 YA MAPINDUZI

Mh Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kwenye picha ya pamoja na ndugu Sigfried Nnembuka ambae ni ofisa wa ubalozi masuala ya siasa ,utamaduni na Mkuu wa kitengo cha Diaspora, Mwenyekiti wa kamati kuu ya Diaspora ndugu Kagutta N.Maulidi, Katibu wa kamati kuu ya Diaspora ndugu Andrew Mhella, Naibu Katibu wa Kamati kuu ya diaspora Ndugu Mwinyimwaka Hatibu na Ms. Judith Joseph Mwenyekiti wa Jumuiya ya Napoli Campania na mjumbe wa kamati kuu ya diaspora

Mh. Mbarouk Nassor Mbarouk Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy, tarehe 25/04/2026 alifanya kikao maalumu na viongozi wa jumuiya za Watanzania pamoja na kamati kuu ya Diaspora kabla ya mkutano wa Watanzania wote wanaoishi nchini Italy.

Mh.balozi pamoja na vikao hivyo viwili pia aliungana na Watanzania katika kusherehekea kumbukizi za miaka 62 ya Muungano.
Katika mkutano wake na Watanzania, Mh Balozi alitoa majawabu ya maswali ya changamoto mbalimbali za Watanzania. Balozi aliwakumbusha Watanzania wote kujisajili katika mtandao wa Diaspora (Diaspora Digital Hub (DDH)https://diaspora.foreign.go.tz/login kwani ni dhamira ya serikali kukusanya data pamoja na kujua idadi ya watanzania wanaoishi nchi mbalimbali duniani, balozi alisema kwa kufanya hivyo itarahisisha serikali kujipanga zaidi katika ushirikishwaji wa diaspora kwenye maendeleo, pamoja na kutoa huduma mbalimbali zenye maslahi kwa diaspora na taifa.

Wakati akijibu hoja za Diaspora, Balozi alisema suala la hadhi maalumu lipo kwenye hatua za mwisho ambapo kilichobakia ni masuala ya kisheria hivyo ni jambo la kusubiri na si la muda mrefu.

Balozi pia aliwaeleza diaspora kwa kifupi hali ya usalama wa nchi kuwa Tanzania imeendelea kuwa salama, yenye amani na utulivu na mshikamano.Pamoja na hali ya kiusalama pia alielezea maendeleo ya uchumi wa nchi unavyoimarika na kukua, hali kadhalika suala zima la mfumuko wa bei ambapo umebaki ndani ya wigo wa makadirio ya serikali. Sambamba la hayo pia balozi alitoa takwimu za pesa zinazoingizwa nchini kutokea kwa diaspora duniani, hivyo serikali inafahamu na kuthamini mchango mkubwa wa diaspora..” alisema balozi”

Mwisho aliwasihi Watanzania kuendelea kuitangaza nchi yao ya asili wakiwa ugenini lakini pia kutafuta fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara. Pamoja na yote hayo Mh Balozi aliwaasa Watanzania kuheshimu Sheria na taratibu za nchi za ugenini kama ilivyo nyumbani.

Katika kuadhimisha sherehe za kumbukizi ya miaka 62 ya Muungano, Balozi Mbarouk aliwakumbusha Watanzania historia ya Muungano wa nchi mbili, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar, alisema Muungano wa tarehe 26/4/1964 uliozaa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wa kipekee duniani na wanapaswa kujivunia na kuulinda.

Mwisho kwa kuhitimisha hotuba yake ya maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano, Mh Balozi alimnukuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan maneno aliyosema kwenye hotuba yake ya maadhimisho ya Muungano mwaka 2024 wakati Muungano ulipotimia miaka 60 kamili...“Muungano wetu umetuimarisha zaidi kama taifa na kwamba Muungano wa Taifa letu unahitajika leo kama ambavyo tuliuhitaji mwaka 1964, hivyo basi hatuna budi kuulinda muungano huu kwa manufaa ya Watanzania wa kizazi cha sasa na Watanzania wa Vizazi vijavyo “Mwisho wa kunukuu.

WUMedia

MATUKIO KATIKA PICHA

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %