
WU®Media
Watanzania 173 waliokuwa wakiishi katika Jimbo la KwaZulu-Natal, Afrika Kusini, wamewasili nchini baada ya kuamua kurejea nyumbani kwa hiari yao.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa ndege maalum kwa ajili ya kuwawezesha raia hao kurejea nchini.
Zoezi la kuwarejesha raia hao limefanyika kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania, kupitia Ubalozi wake nchini Afrika Kusini, na mamlaka husika, huku raia hao wakipatiwa fursa ya kurejea nchini kwa usalama, amani na kwa hiari yao.
Hatua ya Serikali kutoa ndege maalum kwa ajili ya kuwarejesha nyumbani Watanzania hao inaonesha dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwa karibu na Watanzania wanaoishi nje ya nchi, kuhakikisha usalama na ustawi wao, pamoja na kuwawezesha wale wanaotaka kurejea nchini kufanya hivyo kwa utaratibu, usalama na heshima.












