
Na Kagutta NM | WU® Media Italy
Familia yashukuru uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Napoli na Watanzania
Familia ya marehemu Abdallah (MARK) Suleiman Chombo ya mjini Tanga imetuma salamu za shukrani kwa Jumuiya ya watanzania jijini Napoli, Uongozi na Watanzania wote walioshhiriki kwa hali na mali kufanikisha zoezi zima la kuurejesha mwili wa marehemu nyumbani kwa mazishi.
Marehemu Mark Suleiman Chombo alifariki tarehe 17/07/2026 jijini Napoli alipokuwa akiishi kwa takribani miongo mitatu ambapo ameacha Mke na Mtoto wa kiume Ryan Mark Chombo.
Katika salamu hizo ambazo zimetolewa na dada wa marehemu Bi Mariam Suleiman Chombo na kaka wa marehemu ndugu Yusuf Suleiman Chombo, wamesema wametoa shukrani hizo kwa niaba ya familia ndugu jamaa na marafiki lakini kwa niaba ya waislamu na wana Tanga wote kwa ujumla. Katika salamu hizo ndugu hao wa marehemu walitoa shukrani za kipekee kwa Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy, familia imesema Balozi Mbarouk ni mfano bora wa balozi hasa katika kutatua changamoto za Watanzania wanaoishi ughaibuni ikiwa balozi ndie mlezi wa Watanzania wote, wamempongeza na kumshukuru ingawa amefanya yote katika kutimiza wajibu wake lakini familia inasema anastahili pongezi na shukrani.
Familia imewashukuru watanzania na kuwaombea kwa MwenyeziMungu azidi kuwapa moyo wa upendo kwani walichokifanya kimetoa faraja kubwa kwa familia na wana Tanga.
Katika kujibu salamu hizo kwa niaba ya balozi, Mkuu wa kitengo cha Diaspora, utamaduni na siasa ndugu SIGFRIED FILIPO NNEMBUKA amesema shukrani zimepokelewa kwa mikono miwili, lakini amesisitiza kuwa kubwa ni kuendelea kuishi kwa umoja upendo na mshikamano daima na siku zote.
Salamu na shukrani za familia kutoka Tanga Tanzania 👇🏾











