0 0
Read Time:41 Second

Paris FRANCE

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Saidi Yakubu, amekutana na kufanya mazungumzo na Bi. Olivier-Remy Bel, Naibu Mkurugenzi wa Afrika Mashariki katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, katika Ofisi za Ubalozi jijini Paris. Mazungumzo hayo yalihusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ufaransa, hususan namna ya kuendeleza ushirikiano huo kufuatia Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Africa Forward uliofanyika jijini Nairobi, Kenya. Kikao hicho kilitoa fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu vipaumbele vya nchi hizo mbili na namna ya kutumia fursa zinazotokana na Mkutano wa Africa Forward kuimarisha uhusiano na kuendeleza ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote. Ubalozi unaendelea kushirikiana na Serikali ya Ufaransa pamoja na wadau mbalimbali katika kukuza uhusiano wa kidiplomasia na kufungua fursa za ushirikiano kwa manufaa ya Tanzania na wananchi wake.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %