
Na Dr Yahya Msangi
Togo – West Africa
Leo tujifunze njia mbalimbali ambazo magaidi hutumia kupata fedha. Najua somo hili vyombo husika hufundishana. Lakini ni vyema na raia na taasisi zisizo za kiserikali zikajua na kufundisha. Sababu kuubwa ni kuwa katika kutafuta fedha magaidi yanaweza kukutumia wewe binafsi, NGO yako au taasisi yako kupata fedha bila mwenyewe kujua! Kuna watu au NGOs au taasisi zimejikuta matatani kwa kuhusika na kuzalishia magaidi fedha huku zikiwa hazina habari! Watu, taasisi au NGOs wamejikuta wanadakwa na vyombo vya kiusalama kama INTERPOL na polisi au akaunti zinafungiwa! Wengine wamejikuta akaunti zao kwenye mtandao zinafungiwa bila maelezo huku wakichunguzwa kama ni magaidi! Unakuwa umeshawekwa kwenye orodha ya “wanaochunguzwa kwa ugaidi” ila hujui! Utashangaa siku unatafuta visa uende kutibiwa au shughuli zako! Unanyimwa visa bila maelezo ya kina! Au mwanao anaomba scholarship anakutana na kizingiti! Mzazi anachunguzwa kwa ugaidi!
Ndio maana ni vyema ukajua magaidi wanatumia njia zipi kupata fedha ili usije kutumika bila kujua.
Mfano unaweza kutuma mwamala kumbe unasaidia kuchangia kikundi cha magaidi! Ukashangaa mwamala unakuletea balaaa!
PART 2: JE MAGAIDI HUTUMIA NJIA ZIPI KUPATA NA KUSAFIRISHA HELA SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI?
Katika makala ya kwanza nilieleza umuhimu wa kila mtu na kila taasisi kujua jambo hili ili kuepuka kutumiwa au kushiriki kuwazalishia au kuwasambazia hela magaidi. Na ukajikuta kwenye mikono ya vyombo vyenye dhamana. ya kuzuia ugaidi.
Ni vyema pia ukatambua kuwa umoja wa mataifa unao mkataba unaoitwa UN CONVENTION ON TRANSNATIONAL ORGANIZED CRIME (UNTOC) ambao uliridhiwa (adopted) tarehe 15 Novemba mwaka 2000 mjini New York na ukaanza kufanya kazi (entering into force) tarehe 29 Septemba mwaka 2003.
Mkataba huu umeambatana na protokoli 3:
- Protocol to Prevent, Suppress and Punish Trafficking in Persons, Especially Women and Children (inazuia uuzaji watu na haswa wanawake na watoto)
-Protocol against the Smuggling of Migrants by Land, Sea and Air (inakataza kusafirisha wahamiaji kwa njia za ardhini, majini na anga). - Protocol against the Illicit Manufacturing of and Trafficking in Firearms, Their Parts and Components and Ammunition (inakataza utengenezaji silaha, au sehemu ya silaha na milipuko).
Tanzania iliridhia mkataba huu na protokoli zake 3 tarehe 24 May 2006.
Ikumbuke wakati mkataba huu unaandaliwa na kuridhia tatizo la ugadi lilikuwa bado halijawa kubwa. Ugaidi ulipoongezeka ndipo jamii ya kimataifa ikaona ushughulikiwe chini ya mkataba huu. Makao makuu ya sekretariati ya mkataba yako mjini Vienna Austria.
Sasa tuangalie njia wanazotumia magaidi kupata na kusafirisha fedha:
- Njia za kizamani (traditional) mfano utekaji nyara watu
- Njia zisizo za kisasa mfano ‘crowd funding’ ambazo hualika watu wachangie kimtandao.
Katika matumizi ya njia hizi 2 magaidi wanaweza kutfanya hivyo:
- Bila kuvunja sheria aka ktumia njia au taasisi halali
- Kwa kuvunja sheria aka kwa kutuùia njia au taasisi zisizo halali
Kamtihani kadogo!
- Je haiwezekani kuwa tukio la utekaji wa mfanyabiashara maarufu miaka ya hivi karibuni nchini Tanzania lilikuwa tukio la kutafuta fedha kundi la kigaidi?
- Je kujaa wafanyabiashara bungeni na kwenye baraza la mawaziri haiwezi kuwa mbinu ya magaidi kuhakikisha wana njia madhubuti ya kupatia fedha?
- Je haiwezekaniki kuwa kampuni za simu zikawa baadhi ni miradi ya magaidi?
- Je magaidi hawawezi kupachika watu wao kwenye michezo?
Sehemu ya 3 nitaelezea hizi njia haramu na halali kwa kina. Nitatoa na mifano ya jinsi makundi mbalimbali duniani yalivyotumia hizi mbinu kwa mafanikio makubwa mno. Kina IRA, ISIS, Al Qaeda, Al Shaabab, FARC, Red Brigade, n.k.
ITAENDELEAAAAAAAAAAAAAAAA…………..








