0 0
Read Time:2 Minute, 36 Second

Mijadala inayoendelea kwenye mitandao na makundi sogozi ya Wana Diaspora ni Kuhusu Uraia pacha,wapo wanaoona kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano inanyima haki Yao ya Uraia na kwamba sasa umefika wakati Bunge libadili kipengele hicho na kuruhusu Uraia pacha,kwa upande mwingine Diaspora hao hao wapo ambao wanapinga sheria ya Uraia pacha kwa Sababu itakuwa na athari kubwa kwa Taifa na vizazi vijavyo kwa sababu ya kijiografia na usalama wa nchi yetu,hivyo wao wanapendekeza kutungwa sheria ya kuwapa hadhi maalumu Watanzania ughaibuni ambao wamebadili uraia kwa Sababu za kimaslahi binafsi.”

Chini ni mchango wa mawazo wenye vielelezo ulioandikwa na mwana Diaspora nguli wa uchambuzi katika masuala ya kisiasa na kidiplomasia.

Na H.Mkali

mkali@live.co.uk

TATIZO LETU KUBWA NI ARDHI.

Nilichotaka kukisema hapo ni kwamba hayati JPM alianzisha ujenzi wa miradi mikubwa kama vile: Bwawa la Mwalimu Nyerere kule Rufiji, Reli ya kisasa almaarufu kama SGR, Ufufuaji wa Shirika letu la Ndege, Reli na Usafiri wa majini nk nk. Kwenye miradi hii yote hakukuwa na mchango wa moja kwa moja wa kutoka Diaspora.

Ni kweli kuwa Banki Kuu ina takwimu za fedha shilingi takribani bilioni 648 ambazo Wanadiaspora wamepeleka nyumbani. Lakini fedha hizo hazikwenda kwenye miradi ya Taifa kama niliyoigusia hapo juu. Fedha hizi zilipelekwa aidha kwa ndugu na jamaa au kwenye miradi binafsi ya Wanadiaspora wenyewe.

Je, Uraia Pacha usipotolewa Wanadiaspora wa Tanzania tutaacha kusaidia ndugu na jamaa zetu nyumbani?

Mimi ninasadiki kuwa ujenzi wa Taifa utaendelea hata bila ya michango ya kutoka Diaspora. Sisemi kuwa michango ya Diaspora si muhumu. La hasha.

TATIZO NI ARDHI

Hofu yangu kubwa ipo kwenye suala la ardhi.

Napenda kutolea mfano wa jirani ya Kenya.

Kenya hivi sasa ni watu takribani milioni 53.7.(UN estimate 2020).

(1) Katika hawa, watu asilimia 13 (13%) yaani watu wapatao milioni 6.9 hawana ardhi kabisa. (absolutely landless).

(2) Asilimia 67, yaani watu karibu milionj 35.9 wana wastani wa pungufu ya hekta moja (ambayo karibu ni sawa na hakuna).

(3) Zaidi ya nusu ya ardhi yenye rutuba nchini Kenya imehatamiwa na asilimia 20 ya watu.

(4) Kenya haina “full employment or welfare state), yaani Serikali haitowi ruzuku ya kuwakimu watu ambao hawana aridhi ya kulima au hawana ajira.
Hii ndio hali iliyosabisha walichokiita (post election violence) ya 2007/2008. Uchaguzi ulikuwa ni symptom; ugonjwa wenyewe ulikuwa ni uhaba wa aridhi ulikithiri.

Na kwenye makubaliano yaliyoleta usuluhisho wa ile vita ya wao wao; ibara ya nne ilisema: Utaifishaji na ugawaji mpya wa ardhi ni muhimu.

Lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika. Katiba yao Mpya ya 2010 ilichofanya ni kuhalalisha hii hali ambayo si ya haki kwa miaka mingine 99.

Sasa tuwe na Uraia Pacha na Kenya au Jumuiya/Shirikisho lenye kipengere cha “land sharing” hawa Wakenya milioni 42.9 ambao ni jumla ya wasio na aridhi kabisa na wenye pungufu ya hekta moja – kweli
wataacha kuhamia kwetu ambako (kwa sasa kuna aridhi ya kutosha?)

Hiyo ni Kenya tu. Kuna Rwanda, Burundi na Uganda ambako aridhi ni matatizo makubwa sana.

Je, watu wa nchi zote zinazotuzunguka wakiwa na haki ya kuja kuishi Tanzania kwa kutumia tiketi ya uraia pacha, kweli tutakuwa na amani?

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %