0 0
Read Time:1 Minute, 8 Second

Denmark yatangaza kuwa itafunga Ubalozi wake Tanzania

Serikali ya Tanzania imeeleza kusikitishwa na hatua ya Serikali ya Denmark kuamua kufunga shughuli za Ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo mwaka 2024.

Denmark jana ilitangaza uamuzi huo ambao ulihusishwa na mkakati wao mpya wa masuala ya mambo ya nje ambapo mbali na Tanzania pia Nchi hiyo itafunga ubalozi wake nchini Argentina, Ubalozi mdogo wa Chongqing nchini China na ujumbe wa biashara huko Barcelona (Uhispania).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula leo Jumamosi Agosti 28, 2021 ameelezea masikitiko yake kufuatia hatua hiyo ya Denmark hasa ikizingatiwa kuwa hivi karibuni Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikifanya jitihada za kufufua na kuimarisha diplomasia na uhusiano wa Nchi rafiki ikiwemo Denmark.

“Pamoja na hatua iliyochukuliwa na Denmark, ni matarajio ya Tanzania kuwa Serikali ya Denmark itaendelea kushirikiana na Tanzania kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuunga mkono ajenda za Tanzania katika Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na majukwaa mengine ya kimataifa”

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza kwa nia ya mtandao (video conferencing) na Waziri Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Flemming Moller Mortensen kuhusu hamuzi wa Denmark kufunga shughuli za Ubalozi wake Nchini Tanzania
Foreign Affairs Minister Jeppe Kofod in Copenhagen

………………………………………….

Equity Bank ndio mdau namba moja wa Diaspora
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %