0 0
Read Time:1 Minute, 21 Second

WU ® MEDIA

26/02/2022

Balozi wa Tanzania nchi Italy Mh. Mahmoud Thabit Kombo amefanya mkutano Mkubwa na wadau wa NGO”s zipatazo sitini na nne zinazofanya shughuli zake nchini Tanzania.

Balozi wa Tanzania Rome Mh.Mahmoud Thabit Kombo wakati akifungua Mkutano leo alipokutana na wadau wa NGO zipatazo sitini na nne zinazofanya kazi nchi Tanzania.

Katika mkutano huo wa kipekee ambao ulianza saa tatu na nusu asubuhi na kuisha saa kumi na nusu jioni, ulihudhuriwa pia na wadau mbalimbali wa Diaspora ambao pia walipewa nafasi baadhi Yao kujitambulisha, wadau wa NGO walimpongeza Mh Balozi kwa kuwapa nafasi ya kujitambulisha na kutoa fursa ya kuwasikiliza mafanikio yao sambamba na changamoto wanazopitia katika kufanikisha shughulika zao nchini Tanzania.Wadau pia walikiri kuwa ni mara yao ya kwanza kualikwa kukutana na Balozi wa Tanzania Italy na wao kukutanishwa kwa Pamoja.

Pamoja na kuwasikiliza lakini pia Balozi alitumia nafasi hiyo kuwashauri kuwa na ushirikiano wa pamoja ili kuleta ufanisi zaidi kwenye maeneo wanayo yafanyia kazi. Katika mkutano huo Balozi wa Tanzania Rome aliongea mubashara na Balozi wa Italy Tanzania na kumpa fursa ya kutoa salaam zake moja kwa moja kwa njia ya mtandao. Balozi wa Italy nchi Tanzania aliwahakikishia wadau kuwa wapo kwenye mikono salama ya Balozi wa Tanzania Rome na chini ya uongozi wa Mh Rais Mama Samia Suluhu Hassan Tanzania ni nchi salama kufanya shughuli zao.

Mwisho wa Mkutano Mh Balozi Mahamoud Thabit Kombo alipendekeza kuundwa kwa kamati ya Pamoja itakayo simamiwa na mkuu wa utawala wa Ubalozi , Mh. Jubilata E. Shao ambaye ni sehemu kubwa ya mafanikio ya mkutano pamoja na maafisa wengine wa Ubalozi.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %