
KICHWA CHAKAVU CHA TRENI SGR!
1) Kwa Maoni yangu, huu Mjadala kuhusu Kichwa Chakavu (a.k.a. “Kichwa cha Mkandarasi”) unahitaji Majibu ya Kitaalam na ya Kimkataba.
2) Tafadhali rejea hizo Picha za Kichwa Chakavu cha Treni ya SGR (a.k.a. “Kichwa cha Mkandarasi”).
3) Bahati nzuri hakuna ubishi kwamba hicho ni Kichwa Chakavu maana Picha ndio hizo zimemwagwa Mitandaoni na kila Mtu anajua ku-zoom.
4) Niharakishe kusema kwamba mimi siko upande wowote wa Mjadala unaoendelea maana sina Data/Taarifa za kutosha.
5) Naomba tu (kwa kutumia Utaalam na Uzoefu wangu kidogo) kupendekeza Njia Bora kuwaondoa wasiwasi baadhi ya Watanzania wanaodhani labda “tumepigwa” (kwa mara nyingine tena)! Njia Bora ya Serikali yenyewe kujiridhisha kwamba kila kitu kiko sawa (badala ya ku-assume tu kwamba kila kitu kiko sawa)!
6) Ushauri wa Bure kwa Serikali!
a) Nashauri zitumike Tender Documents za Mkandarasi (and Minutes of Contract Negotiations), ambavyo si sehemu ya Mkataba, kucheki iwapo Mkandarasi alisema hiki “Kichwa cha Mkandarasi” kitakuwa kipya au chakavu?! Kitakuwa na Specifications zipi na Bei/Gharama ipi?!
b) Iwapo Tenda inaonyesha Kichwa Chakavu, basi tutamshukuru Mungu.
c) Lakini Tenda ya Mkandarasi ikionyesha Kichwa Kipya (na Bei/Gharama ya Kichwa Kipya), basi huo utakuwa Ushahidi kwamba kumbe kweli tumepigwa.
d) Na iwapo tutakuwa tumepigwa, Serikali itajua nini cha kufanya ikiwa ni pamoja na kuwabana (kuwashughulikia?!) Wasimamizi Wakuu wa Mradi watoe majibu ya Maswali Magumu.
e) Serikali isifanye kosa la kuchukulia haya mambo madogomadogo (“yanayokera masikioni mwa Watawala”!) kirahisi maana wakati mwingine they might be the tip of the iceberg!
f) Baadhi yetu bado tunakumbuka Ufisadi wa TRA kuhusiana na Vichwa vya Treni (na Mabehewa ya Treni). Tulipigwa mchana kweupeee na, kama nakumbuka vizuri, hamna Mtu yeyote aliyechukuliwa hatua stahiki! Eti (baadae) tukaambiwa kuna Vichwa vya Treni bandarini ambavyo hajulikani Mmiliki wake ni nani lakini Serikali imeamua kuvinunua!
g) Hakika Mtu aliyewahi kuumwa na nyoka ana haki ya kuogopa kamba!
7) Narudia!
a) Serikali itumie nafasi hii kujiridhisha na sio tu kufunika kombe mwanaharamu apite.
b) Nadhani ni bora zaidi, Waziri Mkuu mwenyewe akaitisha hizo Tender Documents na Mkataba (Contract Documents) ili acheki mwenyewe.
8) Swali la Kizushi!
a) Naishauri pia Serikali ijiridhishe Mkataba unasemaje kuhusu Umiliki wa Kichwa hiki: Je, Mradi utakapokamilika (baada ya Final Accounts), Kichwa hiki kinakuwa Mali ya Serikali na kinabaki Nchini au Mkandarasi anaondoka nacho kama Mali yake?!
b) Ni lazima Serikali ijiridhishe Mkataba unasemaje.
c) Maana isije ikawa kwenye Tenda yake Mkandarasi alisema wazi kwamba atakodi “Kichwa cha Mkandarasi” kwa ajili ya Majaribio (Testing) na akiondoka ataondoka nacho. Hapo sasa Serikali ijumlishe Gharama za Kukodisha na Gharama za Usafiri kuja na kuondoka Nchini ili ione kama zina-make sense!
9) Kawaida ya Miradi Mikubwa!
a) Kwa wasiojua, kawaida ya Miradi mikubwa kama hii, Mkandarasi huwa ananunuliwa na Mradi (in this case the Government) hata Magari yake yote anayotumia kwenye Mradi.
b) Na yote ni Magari mapya (madogo kwa makubwa, malori na kadhalika).
c) Ukiangalia Tenda yake, utayaona, pamoja na Gharama zake, Specifications zake na Idadi yake.
d) Magari haya huwa ni mapya (brand new), sio chakavu (au re-conditioned).
10) Naendelea kuamini kwamba hiki si “Kichwa cha Mwendawazimu”, bali ni “Kichwa cha Mkandarasi” tu! Ashakum si matusi! Kwamba labda huu ni wasiwasi tu wa aliyewahi kuumwa na nyoka kuogopa kamba! Ndiyo imani na matumaini yangu! Bahati nzuri Serikali haiendeshwi kwa imani…!
11) Ahsante.
12) MUNGU IBARIKI TANZANIA!





BJC. DSM. 23.02.2022. 1118hrs.








