0 0
Read Time:2 Minute, 32 Second

WAKURUGENZI NA UPIGAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
February 22,2022.

Upendo wa Mama yoyote duniani kwa wanae mara zote hauna kipimo!Kila mara Mama anawawazia mema watoto wake lakini sio kila mara watoto wetu wanamuwazia mema Mama yao.

Rais wangu na Mama yangu Samia suluhu Hassan amekuwa mara zote akiwawazia mema watoto wake na wananchi wake na kuamua kuingia kwenye madeni ya mikopo angalau watoto na Tanzania yenye neema ifikiwe Kwa haraka ZAIDI!

“Nitatumia fursa yoyote iliyopo huko duniani kuwaletea maendeleo watanzania”,Mh. RAIS amewahi kusema haya!

Mpaka hapo unaona nia ya Mama ya kukopa kwa lengo ya kuinua maisha ya watoto wake ni njema lakini bahati mbaya Mama ana watoto”Abhaposi” yaani watoto walafi.

Mpaka sasa Mama ameshapigwa na watoto wake pale Mbeya,Iringa,Singida na maeneo mengine mengi lakini bahati mbaya sababu ya “utu” wa Mama, watoto wengine wanajisifu kwa madarasa walijenga kwa haraka haraka na kupendezesha skuli zetu kote Nchini!

Lakini nakwambia ukweli kuwa mpaka dakika hii watoto wameshampiga sana Mama”kwingi”.
Namshauri Mama apite mradi kwa mradi atakutana na vitu vya ajabu sana!

Mama yangu ni mchumi nguli na ni wazi anajua vizuri kitu KINAITWA “Value for Money”!Mama anapaswa akague miradi yake yoote kwa jicho kubwa ZAIDI na Wala asijidanganye kwamba pesa zile za UVIKO za Banki ya Dunia ZAIDI ya Trilioni 3 zimekwenda salama zote!

Mama anapaswa KUFANYA auditing ya nguvu ya haraka KWANI mtaani maneno yameanza hasa baada ya Mama kuonyesha nia ya kutaka kukopa Trilioni 1+ toka WB kwa ajili ya familia yake na watoto wake!

Mama asipofanya hivyo haraka huku mtaani kwetu hanaweza hasieleweke sana!Maneno ni mengi nikaona nimshauri Mama yangu!Watu wanasema “mipango sio matumizi” yaani wakati wewe unapanga mazuri kwa ajili ya maendeleo ya watu wako!

Lakini watoto wako “Abhaposi” yaani walafi wengine, wanawaza kuitumbua mikopo yako!kelele hizi za huku mtaani sio nzuri kwetu na hasa Mimi mwanao wa kwanza ambaye unajua jinsi nilivyojitoa na ninavyopambana kuelezea mazuri yako unayofanya NDANI ya familia yako ya Tanzania!

Mama yangu kipenzi,moja ya ajenda ambayo inaweza kutuchafua sana sisi kama familia mwaka 2025 inaweza ukawa ajenda ya matumizi ya mikopo uliyotukopea sisi watoto wako!

Mama tuna options mbili kwa sasa(I)kuitisha kikao cha familia na kila mwanao”Wakurugenzi” na waseme kwa uwazi kabisa mbele yako jinsi alivyotumia zile FEDHA zako za UVIKO 19 za WB bila kujali uzuri wa madarasa yake aliyojenga na mwishowe uwaulize kila mmoja akupe “chenji Yako kama IPO”.MBONA wakati ule wakati wa Baba walikuwa wanarudisha “chenji zenu?”why not now?

(II)Baada ya hapo waambie Watanzania kwanini usikope tena?Hakuna ambaye hatokuelewa na kila mtu atafurahia mikopo yako!

Watu wenye akili wameshajua kuwa tatizo hapa sio mkopo wala mkopaji yaani wewe Mama!Tatizo hapa ni sisi watoto wako!

Ile kauli yako ya “..Mimi Mama wewe mtoto,โ€ฆukinizingua nakuzingua ..” lazima ianze kututisha sisi watoto wako!

Mimi mwanao na kifungua mimba”tumbo” wako nimeamua kusema maana kelele za wenzangu “Mainzi” zimekuwa nyingi sana na anayenisumbua sana huku shuleni ni huyu jirani MASOUD KIPANYA!

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %