WU® Media PRODUCTION
MKUTANO MKUBWA WA UTALII DUNIANI KUFANYIKA TANZANIA
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesaini Mkataba wa Tanzania kukubali kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi Oktoba, 2022. Mkataba huo umesainiwa jijini Madrid nchini Hispania mbele ya Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Bw. Zurab Pololikashvil.









