0 0
Read Time:2 Minute, 31 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

DARASANI KWA DR YAHYA MSANGI

Mara kadhaa utasikia vijana wakisema “Bora vita ije tuheshimiane”! Hawajui vita ni nini sio kosa lao. Umri na kutokusoma historia ya vita mbalimbali Ndiyo tatizo.

1978 BABA WA TAIFA AKIJADILI JAMBO NA MAKAMANDA KUHUSU HALI YA UWANJA WA MAPAMBANO WAKATI WA VITA VYA KAGERA


Ni katika vita watu walikatana vichwa na kungoana meno na kupeleka kwao! Léo ni Watu haohao wanatuambia Biashara ya binadamu au viungo vya binadamu ni uhalifu. Hawaoni haya kuturidishia vichwa na meno na tulivyo wahovyo tunafurahia!

Ngoja nikujuze baadhi tu ya mambo yaliyotokana na vita:

  1. Viuatilifu vya kilimo (agrochemicals). Asili haikuwa kujua magugu (herbicide), wadudu (insecticide), kuharakisha au kudumaza ukuaji (plant growth regulator), n.k. Asili ilikuwa kumshinda adui vitani. Vita za Anglo Saxons, Ottoman, Crusades, Vietnam ni kati ya vita vilivozalisha na kutumia agrochemicals sana. Mifano: kuangamiza misitu ili adui akose pa kufichama, kuzuia maadui wasizaane, kusababisha adui wazae walemavu, mamba kuporomoka, n.k. Agent Orange ni herbicide iliyotumika sana Vietnam n’a hadi Leo watoto wanazaliwa walemavu. Tanzania tuliitumia sana kwenye mashamba ya Ngano (BASUTO WHEAT COMPLEX). Wenyeji wa Hanang, BASUTO, Mulbadaw, nk. wataikumbuka. Ilikuwa ikinyunyizwa anga na ardhi inakuwa njano tupu!
    Kwa hiyo ni BAADA ya vita Ndiyo sumu Hizi zikapatiwa KAZI mpya. Ukumbuke madhara ni yaleyale yaliyokusudiwa kwenye vita!
  2. Ni katika vita ilizuka dhana ya ubora baina ya binadamu. Baadhi ya binadamu wakawa bora kuliko Wenzao. Mfano: ikiwa wéwé ni taahira ikawa ruksa utumike kutibu askari au kufanyia utafiti. Mfano askari kapoteza Figo wanachukua ya taahira wanampa askari. Ubora wa binadamu ukapimwa kwa kigezo cha mchango wake kwenye vita. Kama huna mchango Unaweza kufanyiwa lolote kama kunyimwa chakula, kufanyishwa kazi bila mshahara, mkeo kuchukuliwa kustarehesha askari n.k.
  3. Mwanamke kuwa kiumbe daraja la 2. Wanawake n’a watoto hawakuruhusiwa Kwenda vitani. Kazi kubwa ya wamama ikawa kushona uniform za askari, kustarehesha askari, kuangalia watoto, n.k. Vita ndio hasa vilisimika mfumodume. MPAKA Leo Wapo ndugu wa Wamama waliotumika kustarehesha askari wanadai fidia nchi mbalimbali. Wapo watu kwa mamilioni walizaliwa kwenye utaratibu huu!.Sasa ni wazee. Hâta mababu zetu walioenda Burma walishiriki!
  4. Kudhulumu wafanyakazi. Ni katika vita Ndiyo waajiri walipewa ruksa ya kutowalipa mishahara wafanyakazi. Jukumu lao KUBWA likawa kuzalisha bidhaa zinazohitajika vitani. Watawala hawakujali wanazalishaje. Forced labour (Ajira ya kulazimishwa) ikashamiri. Utake usitake utafanya kazi Usipoenda kazini mwajiri anatoka taarifa polisi! Polisi watahamikisha unaenda kazini. Na ukileta jeuri utashitakiwa kwa kosa la usaliti.
  5. Matumizi ya mikorogo: ni katika vita ilikuwa muhimu kuficha sura. Ukawa muhimu pia kujitibu chawa, papasi, kunguni, mmba, n.k. Wati wakalazimika kutumia mikorogo. Mfano mzuri ni matumizi ya sumu ya DDT. Chawa, kunguni, papaso na mmba vilikithiri mno enzi za vita. Wati wakawa wanaoga DDT! DDT iliwaondolea utitiri, Chama, n.k. Lakini ikawaachia cancer! Ukawa Sababu matibabu ya wenzetu KUPIGA marufuku DDT! Sisi Bado tunalazimishana kuiupuliza kuulia mbu! Ingawa tumeipiga marufuku kwenye kilimo bado inatumika sana! Watu hawajui na wizara haidhibiti kisawasawa!
Vita kuu ya kwanza ya dunia

Haya ni baadhi ya madhara ya vita!

Je bado tupigane ili tuheshimiane? Vipi Ukraine? Tupigane vita kuu nyingine?

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %