
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
USIKUBALI KUPOTOSHWA KUHUSU LOLIONDO NA PORI TENGEFU LA NGORONGORO.
✍🏼Wapo baadhi ya Watanzania wanaojiita watetezi wa Haki za Binadamu, wamekuwa na tabia ya hovyo ambayo ina lengo la kuichafua Serikali na Nchi yetu Tanzania na imekuwa ni kawaida yao kupotosha Umma kwa kueneza habari za Uongo.
✍🏼Wamekuwa wakitumika kwa Maslahi yao binafsi, wanatumia Kurasa zao za Mitandao ya Kijamii kushawishi na kueneza Uongo dhidi ya hali ya Ngorongoro lengo lao kubwa ni kuichafua Serikali kwa kutangaza UONGO na kuichonganisha Serikali na wananchi wake waliokuwa wakiishi Loliondo na Ngorongoro.
✍🏼Hali ya Maeneo hayo mawili ni Shwari na Salama, wananchi kwa Hiari yao wameitikia wito wa Serikali Kuhama katika maeneo hayo na kuhamia Msomero Wilayani Handeni Mkoani Tanga ambako Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imewajengea Makazi Mapya ambayo yamekuwa na huduma zote muhimu kwa binadamu.
✍🏼Wananchi walihama kwa hiari yao Ngorongoro na kuhamia Mkoani Tanga wanafurahia Maisha katika Makazi yao Mapya, Maisha wanayoishi huko ni yakisasa Shughuli zao za Kijamii zinaendelea kama kawaida bila kikwazo chochote.
WAEPUKE WAPOTOSHAJI WANAOJIITA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU HALI YA KUWA NI WAGANGA NJAA








