
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
August 20,2022.
Kuna uwezekano mkubwa kuwa ifikapo Mwaka 2035 neno ndoa ndani ya Nchi ya Tanzania litakuwa ni msamiati na sio ishu tena baada ya jamii kushuhudia ongezeko kubwa la ndoa kuvunjika lakini ni kama jamii imekaa kimya kana kwamba hakuna kinachoendelea.
Akiwa katika uzinduzi wa kambi ya vijana ya wasabato Mkaoni Dar es salaam hivi karibuni,Waziri George Simbachawene alishangazwa na idadi ya ndoa karibia 350 kuvunnyika ndani ya miezi sita ya uwepo wake katika Wilaya moja tu Nchini ambayo ni Wilaya ya Temeke,Jijini Dar es salaam!
Sababu kubwa miongoni mwa sababu nyingi zinazotajwa kusababisha kuvunjika kwa ndoa nyingi Nchini kwa sasa, ni uwepo wa(i) Wanaume na Wanawake ambao wanaingia kwenye ndoa huku nao wakiwa wametokana na familia ya mzazi mmoja maarufu kama “single mother family”.
Sababu ya pili inayotajwa kupelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi Nchini ni vijana wa sasa, Waume kwa Wanawake kutoandaliwa vizuri katika misingi ya kuwajibika katika ndoa,kuheshimu ndoa pamoja kiburi na kukosa hofu ya Mungu wakati wa makuzi yao!
Ndoa nyingi kwa sasa zinakosa Wanawake wale wenye kujitoa kwa asilimia mia moja katika kulinda,kutetea na hata kuvumilia changamoto za ndoa ambazo zinatajwa kuwa ni changamoto za mpito tu kwenye taasisi ya ndoa!
“..mwanamke mpumbavu uvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe”,Bwana Mungu asema!
“..enji wanaume wapendeni wake zenu na enyi wanawake watiini waume zetu…”.Bwana asema!
Serikali ya Mama yangu Samia Suluhu Hassan, inapaswa kuliangalia tatizo hilo kama tatizo la kimaendeleo”developmental problem” kama yalivyo matatizo mengine ya kimaendeleo katika Taifa hasa ukizingatia Rais wetu Mama Samia anabeba nafasi ya Mama wa Taifa na Bibi pia!Rais anahitaji sasa apate angalau takwimu za haraka haraka kuhusu tatizo hili na kuona ukubwa wa tatizo kwa Nchi nzima ukoje!
Wote tunajua kuwa msingi wa Taifa lenye maaduli,heshima na malezo bora ya kidini na kijamii uanzia kwenye familia na suala hili linapaswa kubebwa kama ajenda ya kitaifa kwani bila kufanya hivyo,natabili miaka ishirini ijayo Taifa litakosa kitu kinaitwa familia kwa maana ya uwepo wa Baba na Mama ndani ya paa moja la nyumba!Hii ni hatari!
+2557466484.








