
Read Time:2 Minute, 4 Second
ITALY -TANZANIA BUSINESS AND INVESTMENT FORUM
WU® MEDIAPRODUCTION LIMITED

Kongamano hili kubwa la kibiashara na uwekezaji linakwenda kufungua fursa kubwa za kibiashara baina ya nchi hizi mbili yaani Italy na Tanzania na Hilo liko wazi baada ya kupata muitikio mkubwa wa wafanya biashara wa pande zote. Mgeni rasmi katika kuhitisha siku ya leo ni Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Mh. Ashatu Kijaji ambae amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwenye kongamano hili kubwa la aina yake.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ametoa wito kwa Watanzania kutoa maoni kuhusu maboresho ya sheria mpya ya uwekezaji ambayo ilisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa nane wa Bunge.
Amesema sheria hiyo sasa imepelekwa kwa wananchi ili nao watoe maoni yao ya kuiboresha, lengo likiwa ni kuifanya ifae kutumika kwa maendeleo ya Taifa.
Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kwa dhati kuwalea vema wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, ndio maana amepunguza kiasi cha fedha alichotakiwa kuwa nacho mwekezaji ili aweze kujisajili katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Waziri huyo wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara amesema
awali mwekezaji alitakiwa kuwa na dola laki moja za kimarekani ili ajisajili, ila sasa atapaswa kuwa na dola elfu hamsini tu.
Amesema kutokana na juhudi za serikali katika kuimarisha diplomasia ya kiuchumi baina ya Tanzania na mataifa ya nje, kumekuwa na matokeo chanya katika sekta ya biashara ambapo hivi sasa kampuni za uwekezaji takribani 40 kutoka Italia zimeshiriki katika jukwaa hilo la Biashara na Uwekezaji linalounganisha wafanyabiashara wa Tanzania na Italia.
Kwa mujibu wa Dkt. Kijaji, hadi sasa uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni mbili za kimarekani umeshafanyika hapa nchini kutoka kwa kampuni za nchini Italia.
























