0 0
Read Time:49 Second

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema uanzishwaji wa Mahkama maalumu ya rushwa na uhujumu uchumi itaisaidia Serikali katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi na rasilimali za umma.

kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar

viwanja vya Mahakama Kuu ya Zanzibar

Aidha, Rais Dk.Mwinyi alieleza kufarijika kwamba tayari kamati ya wataalamu imeundwa kusimamia na kuratibu mchakato wa kuanzishwa kwa Mahkama hiyo

Ameyasema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar viwanja vya Mahkama Kuu ya Zanzibar, Tunguu, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Katika maadhimisho hayo Rais Dk.Mwinyi amezindua Bendera na Nembo rasmi ya Mahkama ya Zanzibar na kupokea ripoti ya utendaji kazi wa Mwaka 2022.

Alisema Serikali itatoa kipaumbele kikubwa katika bajeti yake kwenye matumizi ya Tehama na uimarishaji miundo mbinu ya taasisi za Sheria nchini.

13 Februari 2023,

Viwanja vya Mahkama Kuu Zanzibar,Mkoa wa Kusini Unguja.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %