
WU® MEDIA
Na Mwandishi wetu, NAPOLI

Pichani: Marehemu Bakari Shabani Bakari
Siku ya Alhamisi ya tarehe 1/03/2023, Mjini Napoli Watanzania walikusanyika kwa Pamoja kukamilisha mchakato wa kupeleka mwili wa mpendwa wao, mwana Diaspora mwenzao aliyefariki tarehe 15/02/2023 jijini Napoli Italy. Marehemu Bakari Shabani alifariki akiwa hospitalini ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Siku ya Jana iliyogubikwa na simanzi na Majonzi kwa Watanzania, ilikuwa ni siku ya kukamilisha taratibu za Maombi na Sala tayari kwa mwili kuondoka siku ya ijumaa kuelekea Tanzania kwa mazishi. Kwa taarifa tulizonazo ni kwamba marehemu atazikwa mjini Tanga.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy Mh Mahmoud Thabit Kombo, kutokana na majukumu makubwa ya Kazi aliweza kutuma ujumbe wa maofisa wa Ubalozi ambao walimuwakilisha kuja kuungana na Watanzania mjini Napoli katika Maombi, Dua na sala, kumuaga marehemu Bakari Shabani Bakari.
Wakati akitoa salaam kwa niaba ya Balozi, ofisa wa Ubalozi Ndugu Nnembuka, alieleza jinsi gani walivyo guswa na msiba, kwa niaba ya Balozi aliwapongeza Watanzania wote Kupitia Jumuiya zao kwa ushirikiano Mkubwa walionyesha katika kuchangia shughuli na gharama zote za msiba, Mh Nnembuka aliendelea kusisitiza mshikamano, umoja na upendo baina ya Watanzania wote , na ameahidi kwa niaba ya Balozi kuwa, Ubalozi utaendelea kushirikiana na Jumuiya za Watanzania kwa karibu. Mwisho kwa kipekee alipongeza uongozi wa Jumuiya ya Watanzania NAPOLI ukiongozwa na Mwenyekiti wake Dada Judith Joseph Njozi kwa Kazi kubwa wanazofanya na jinsi walivyoweza kuongoza zoezi zima la msiba mpaka kufanikisha.
Baadhi ya Watanzania waliongea machache kuhusu marehemu Beka Chavalia kama alivyofahamika , ucheshi wake na ukaribu na watu wengi.
click Instagram link



















