0 0
Read Time:1 Minute, 1 Second

WU® MEDIA

MBAKAJI THABO BESTER

Jeshi la Polisi Tanzania limethibitisha kuwa Makachero wa Tanzania wamewakamata Raia wa Afrika Kusini, Thabo Bester maarufu kwa jina la ‘Mbakaji wa Facebook’ na Mpenzi wake Dr. Nandipa Magumana pamoja na Zakaria Alberto.

Dr Nandipha Magudumana

Inadaiwa watatu hao wamekamatiwa Arusha japo taarifa rasmi Ya Polisi haijasema eneo walikokamatiwa ,kwa upande mwingine Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi, David Misime amesema taratibu za mawasiliano ya kisheria ya ndani na ya kimataifa zinaendelea kukamilishwa.

Itakumbukwa kuwa Thabo amekuwa akisakwa na Polisi wa Afrika Kusini akikabiliwa na kosa la kughushi kuwa amefariki alipokuwa gerezani na kutoroka kisha baadaye ikabainika kuwa hajafariki, kitendo ambacho kiliishangaza Nchi nzima.

Mamlaka iliamini kuwa Thabo Bester alifariki baada ya kujichoma moto katika Gereza la Hloko Jijini Bloemfontein May 2022 lakini baadaye ikabainika mwili uliodaiwa ni wa Thabo haukuwa wake ambapo mwanzoni mwa mwezi huu Polisi Afrika Kusini walianzisha msako mkali wa kumtafuta.

Thabo alidaiwa kuwarubuni Waathiriwa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kisha kuwabaka na kuwaibia ambapo mwaka 2012 alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la ubakaji, wizi na mauaji.

Read

https://www.news24.com/news24/southafrica/news/thabo-bester-nandipha-magudumana-arrested-in-tanzania-found-with-multiple-passports-20230408

#WU®MEDIAUPDATE

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %